The House of Favourite Newspapers

Gomes Amfungukia Morrison

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amefunguka kuwa kiungo mshambuliaji wake, Bernard Morrison ni ‘Super Sub’ kutokana na uwezo mkubwa wa kusoma mbinu za wapinzani na kubadilisha mchezo ndiyo sababu kubwa ya kumuanzisha benchi.

 

Katika michezo miwili iliyopita ambayo Simba ilicheza dhidi ya Dodoma Jiji na Kagera Sugar, Morrison alionesha kiwango kizuri na kufanikiwa kuifungia Simba bao moja, huku zote akitokea benchi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema: “Tunapenda kumtumia Morrison akitokea benchi kwa kuwa ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kusoma namna ambavyo wapinzani wanacheza na kufanya maamuzi sahihi ya kuvunja ukuta wao.

 

 

“Amekuwa katika kiwango bora kwenye michezo miwili iliyopita na hili ni jambo zuri hasa kwa kuwa tunaelekea katika michezo mikubwa mfululizo, kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga na ile ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs.

Leave A Reply