Kartra

Gomes Ampa Mapumziko Maalum Luis Simba

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes ametoa mapumziko ya siku nne kwa baadhi ya nyota wake akiwemo Luis Miquissone.

 

Hiyo ni baada ya kumalizika kwa mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri uliochezwa Jumanne iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 lililofungwa na Miquissone baada ya kugongeana vizuri na Mzambia Clatous Chama.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Gomes alisema mapumziko hayo waliyaanza Jumatano yatamalizika Jumamosi na kuanza mazoezi pamoja na wenzao.

 

Gomes alisema kuwa wachezaji wake hao walitumia nguvu nyingi katika mchezo huo dhidi ya Ahly zilizowawezesha kupata ushindi huo na kukaa kileleni katika msimamo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa na pointi 6.

 

Aliongeza kuwa katika mchezo wao wa jana wa Kombe la FA alitarajia kuwatumia wachezaji ambao hawakucheza mechi ya Al Ahly ili kutoa nafasi ya kupumzika.

 

“Nimetoa nafasi ya mapumziko kwa wachezaji wangu waliocheza mchezo wa Ahly ambao mchezo wa FA dhidi ya African Lyon hawatakuwepo.“Nimepanga kuwatumia wachezaji ambao hawakucheza mchezo huo, lengo ni kutoa nafasi ya kupumzika na wengine waliokaa benchi na wasiokuwepo kabisa nao kucheza,” alisema Gomes.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam


Toa comment