Kartra

Gomes: Tupo Tayari Kwa Yanga

KUELEKEA mechi ya Kariakoo Dabi kati ya Simba na Yanga inayotarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema wamejiandaa vizuri, hivyo mashabiki wanapaswa kujitokeza kwa wingi uwanjani kutoa sapoti kwao.

Gomes, raia wa Ufaransa, hii itakuwa dabi yake ya kwanza dhidi ya Yanga baada ya kukabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo Januari 24, mwaka huu.Simba ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara hivi sasa wakiwa na pointi 61, watakuwa wenyeji wa Yanga ambapo mechi ya mzunguko wa kwanza ilimalizika kwa sare ya 1-1.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Gomes alisema: “Tumejiandaa vyema, masuala ya kushinda au kushindwa yataonekana hiyo tarehe nane, mje muone kama tutachukua ushindi au la.

STORI: CAREEN OSCAR,Dar es Salaam


Toa comment