The House of Favourite Newspapers

GSM  Wazindua Shoexpress Dodoma

0
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri mkuu,Sera,Bunge,Kazi Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde (kushoto), akimsikiliza Meneja Mkuu Msaidizi wa  GSM Mall, Ahmed Eriba, akimuelezea ubora wa viatu wakati wa uzinduzi wa duka la viatu la Shoexpress jana lililopo jijini Dodoma.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group, Matina Nkurlu, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana wakati wa uzinduzi wa duka la viatu la Shoexpress jana lililopo jijini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde , na Meneja Mkuu Msaidizi wa GSM Mall, Ahmed Eriba.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde (kushoto), akimsikiliza Meneja Mkuu Msaidizi wa  GSM Mall, Ahmed Eriba, akimuelezea ubora wa viatu wakati wa uzinduzi wa duka la viatu la Shoexpress jana lililopo jijini Dodoma.  Katikati ni Meneja Mkuu, Inam Soudagar.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde (katikati), na Meneja Mkuu Msaidizi wa GSM Mall, Ahmed Eriba, wakikata keki wakati wa uzinduzi wa duka la viatu la Shoexpress jana lililopo jijini Dodoma.  Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group, Matina Nkurlu.

KAMPUNI ya GSM Group jana  Februari 14, mwaka 2020, ilizindua duka kubwa la kuuza viatu vya kisasa na vyenye ubora wa hali ya juu linalopatikana Shoppers Plaza, jijini Dodoma.

 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, aliipongeza GSM Group kwa kuwafikiria wakazi wa Dodoma kuwapelekea bidhaa hizo za kiwango
cha juu.

Alisema kuwa Serikali inafarijika kuona wawekezaji wakizidi kupanua wigo katika biashara zao ili kuwafikia Watanzania kokote walipo na si Dar es Salaam pekee kama ilivyozoeleka.

“Nawapongeza sana GSM Group kwa kuwaletea wakazi wa Dodoma duka hili la viatu vyenye ubora, angalau wanaungana na Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli katika kuifanya Dodoma kuwa na hadhi ya Jiji, lakini pia makao makuu ya nchi.

 

“Tunafahamu kuwa pamoja na kuwaletea wakazi wa Dodoma bidhaa hii ya viatu, pia  duka hili litatoa fursa ya ajira kwa wananchi wa jiji hili. Tunawaomba muendelee kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu maana tulizoea kuona maduka ya
aina hii yakifunguliwa Dar es Salaam pekee,” alisema.

 

Aliwataka wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kujipatia vitu na bidhaa nyingine katika duka hilo. Kwa upande wake, Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM, Matina Nkurlu, alisema kuwa duka hilo litafahamika kwa jina la Shoe Express ambapo litakuwa na viatu vyenye  ubora wa hali ya juu vinavyolingana na hadhi ya jiji hilo la Dodoma.

 

“Viatu vitakavyopatikana katika duka hili ni vya kiwango cha kimataifa, vikiwa na bei ya kawaida kabisa kuwawezesha wakazi wa Dodoma na wengineo kuimudu,” alisema Nkurlu.

 

Alisema mbali ya duka hilo, GSM Group imedhamiria kuendelea kuwekeza katika jiji hilo ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt, John Pombe Magufuli kuifanya Dodoma kuwa na mwonekano wa makao makuu hasa ya nchi.

 

GSM Group wana maduka makubwa ya nguo za watu wa rika na jinsi zote, vifaa vya michezo, samani za ndani, vifaa vya umeme na ujenzi na nyinginezo yanayopatikana katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Leave A Reply