The House of Favourite Newspapers

GSM Yawamwagia Mamilioni Kwa Morrison

0

MDHAMINI wa Yanga ambaye ni Kampuni ya GSM imeendelea kuonyesha kufuru zake na safari hii imewafanyia sapraizi wachezaji wake wote kwa kuwafanyisha shopping yenye thamani ya Sh Mil 17.

 

 

Shopping hiyo imewahusisha wachezaji wote 28, waliosajiliwa na timu hiyo kwenye msimu huu akiwemo mshambuliaji mkongomani David Molinga ambaye ameshafunga mabao nane kwenye timu hiyo na wengi walikuwa wanafahamu kuwa yupo nchini Ufaransa, lakini ghafla akaibukia ofisi za GSM.

 

Molinga kabla hata ligi haijasimamishwa alikuwa ameomba ruhusa ya kwenda nchini kwao, lakini juzi alionekana akiwa mmoja kati ya wachezaji waliotua GSM kufanya shooping hiyo.

 

 

Shopping hiyo ya mastaa hao walifaya kwenye duka kubwa la GSM la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa kila mmoja kupewa vocha yenye thamani ya Sh 600,000 (kwa wachezaji 28 ni sawa na milioni 16.8) kwa ajili ya kujipatia bidhaa mbalimbali dukani hapo na maduka mengine ya hapa nchini akiwemo staa wao Bernard Morrison ambaye amekuwa moto kwa sasa.

 

 

Akizungumza na Championi Jumatano, nahodha msaidizi wa timu hiyo, Juma Abdul alithibitisha hilo kwa kusema kuwa juzi walipigiwa simu kutoka kwa meneja wao, Abeid Mziba na kutakiwa kufika Mlimaini City bila ya kujua kitu wanachokwenda kufanya na walipofika wakakutana na sapraizi hiyo.

 

Abdul alisema kuwa jana ilikuwa awamu ya kwanza ya wachezaji kupata vocha hizo ikihusisha wachezaji tisa pekee ambao ni Haruna Niyonzima, Juma Abdul, Vincent Chikupe, Papii Kabamba Tshishimbi, Metacha Mnata, Ally Mtoni, David Molinga, Japhary Mohamed na Kelvin Yondani.

Aliongeza kuwa awamu ya pili inatarajiwa kuendelea leo Jumatano, itakayowahusisha wachezaji wengine tisa watakaofika Mlimani City kwa ajili ya kupewa vocha zao za kufanya shopping.

 

 

“Tuanze kwa kuwashukuru Kampuni ya GSM ambao ndiyo wadhamini wetu Yanga kwa hiki kitu kikubwa walichokifanya kwetu wachezaji, kwani hakijawahi kufanyika, hii ni mara ya kwanza.

 

 

“Kwetu wachezaji tunajisikia faraja na kuona umuhimu wa udhamini wao ndani ya Yanga, hivyo hii ni awamu ya kwanza kwetu kwenda Mlimani City na kupewa vocha hiyo yenye thamani ya Sh 600,000 kila mchezaji.“Nyingine itaendelea kesho (leo) kwa wachezaji kufika hapo kuchukua vocha zao, kwa wachezaji waliokuwepo nje ya Dar, wenyewe watapatiwa mara baada ya kurejea hapa,”alisema Abdul.

Leave A Reply