The House of Favourite Newspapers

Guinea: Mechi ya Kimataifa Yaahirishwa

0

Kufuatia machafuko nchini Guinea, mchuano wa timu ya taifa hilo wa kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Morocco nyumbani uliofaa kuchezwa jana umeahirishwa. Shirikisho la soka duniani Fifa limesema uamuzi huo ulichukuliwa ili kulinda usalama wa wachezaji na maafisa wa mechi.

 

Timu ya Morocco imenaswa nchini hmo baada ya mapinuzi hayo na inaripotiwa kungoja kupata idhini ya ubalozi kusafiri hadi uwanja wa ndege.

 

Rais Conde alichaguliwa kwa muhula wa tatu uliokumba na utata ambao ulisababisha ghasia mwaka jana .Mwanasiasa huyo mkongwe alichaguliwa mara ya kwanza kuwa rais mwaka wa 2010 katika uchaguzi wa kwanza ulioshuhudia makabidhiano ya mamlaka ya njia ya Amani.

 

Licha ya utawala wake kufanikiwa kuboresha hali ya uchumi amelaumiwa kwa kuongoza serikali inayokiuka haki za binadamu na unyanyasaji wa wakosoaji wake.

Leave A Reply