The House of Favourite Newspapers

Guinness Smooth Yapeleka Fursa Mpya Kanda ya Kaskazini

0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakiifurahia bia mpya ya Guiness smooth muda mfupi baada ya kuzinduliwa jana jijini Arusha.

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imeendelea kupanua wigo wa bidhaa zake sokoni baada ya kuzindua bia mpya aina ya Guinness Smooth katika mikoa ya Moshi, Arusha, Manyara na Tanga.

Katika uzinduzi wa bia hiyo mpya, wateja wa kampuni ya SBL, wauzaji wake wa bia pamoja na wenye mabaa walipata nafasi ya kuonja na kufurahia ladha ya kipekee ya bia ya Guinness smooth.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo jijini Arusha, Meneja Uvumbuzi wa SBL Bertha Vedastus alisema “Bia hii mpya kwenye familia ya Guinness ina ladha ya kipekee ambayo inamfanya kila mnywaji afurahie kila mara anapoitumia na wakati akiwa na marafiki,” alisema

Baadhi ya wageni ambao ni wauzaji na wasambazaji wa bia mkoani Arusha wakifurahia bia mpya ya Guiness smooth wakati wa uzinduzi wa bia hiyo inayotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya bia ya Serengeti.

Bertha aliongeza “Ikiwa imetengenezwa kwa kumjali mnywaji wa Kitanzania, bia hii ina hadhi ya kimataifa na imetengenezwa katika kiwanda chetu cha moshi huku ikitumia malighafi za Kitanzania ikiwa ni Pamoja na shayiri inayolimwa katika mikoa ya Moshi, Arusha na mingineyo,”

Meneja uvumbuzi huyo aliongeza kuwa familia ya Guinnness Tanzania inayo furaha kuwaletea bia hiyo wakazi wa mikoa ya Kaskazini ambao siku zote wamekuwa waaminifu kwa bidhaa za SBL nakuongeza kuwa bia ya Guinness smooth itakuwa ikipatikana kwa shilingi 1,500 tu.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakisakata rhumba muda mfupi baada ya uzinduzi uliofana wa bia mpya ya Guinness smooth uliofanyika katika Hotel ya Mount Meru jijini Arusha na kuhudhuriwa na wasambazaji pamona na wauzaji wa bia.

“Guinness ina historia ndefu na kongwe ya kutengeneza bidhaa ambazo zimefanikiwa kuteka soko la dunia nakuendelea kuwa kinara. Bia hii ni muendelezo wa Guinness kuwaletea wateja wake bidhaa ambazo zinakidhi mahitaji yao na kuenda na wakati,” alisema.

Baadhi ya wateja waliohudhuria uzinduzi na kuonja bia hiyo mpya walielezea kuvutiwa na ladha ya kipekee ya bia hiyo mpya na kusema kuwa watakuwa mabalozi wazuri.

“Bia ni nzuri na huu ni ujumbe kuwa iko kila sababu ya kufanya vizuri sokoni. Kwangu mimi kama msambazi wa bia naona ni fursa ambayo nitaitumia vyema kwaajili ya kuweza kuongeza wigo wa wateja wangu Pamoja na kukuza biashara yangu pia,” alimaliza kusema.

Leave A Reply