The House of Favourite Newspapers

Gunze Atoboa Siri COSOTA Kuhamishwa Wizara – Video

0

MWENYEKITI wa Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Kahabi Gunze amesema athari iliyokuwepo kwa COSOTA kuwa Wizara ya Viwanda ni mahusiano na kwamba chama hicho kilikuwa kikiwajibika kwenye wizara hiyo na si Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 

Gunze amesema hayo leo Alhamisi, Julai 16, 2020, wakati akifanya mahojiano na kipindi cha front page kinachoruka kupitia +255 Global Radio na kuongeza kwamba changamoto kufanikisha mambo yao hasa mirabaha ya malipo ya kazi zao, kulikuwa na shida.

 

“Baada tu Rais kuniteua kuwa Mwenyekiti wa BASATA niliandika waraka nikasema maoni yangu kuhusu BASATA, COSOTA na Bodi ya Filamu kuwa chini ya chombo kimoja au wizara moja. Juzi Mhe. Rais Magufuli alivyoagiza COSOTA ihamishiwe wizara ya Sanaa nilishangilia sana.

 

“Kuna sheria ya COSOTA, ipo ya Bodi ya Filamu na kuna sheria ya BASATA, hizi ni sheria za vyombo tu, lakini hakuna sheria ya tasnia nzima ya sanaa. Je, sanaa inafanyaje kazi, vitu gani vimo ndani ya tasnia ya sanaa? hapo ndipo kuna shida.

 

“Huko mbele tutaweka mfumo, chombo cha habari kikipiga muziki wa msanii mfano dakika 90 kwa siku, kitawekwa kifaa na formula kitaonyesha huo muda na pesa ambayo utamlipa msanii kulingana na muda ambao utakuwa umecheza muziki wake kwa siku.

 

“Tumeanza na Bodi ya Filamu kupunguza gharama za usajili kutoka laki 5 mpaka elfu 50, ili laki 4.5 watumie kutengeneza kazi zao. Kwenye kuwalipa wasanii kulingana na unavyopiga muziki wake tutakaa na wasanii na TV na Radio stations kisha tutakubaliana pamoja.

 

“Ili wasanii wapate mrahaba kwanza lazima ujisajili BASATA na kisha COSOTA, vyombo hivi vitafuata taratibu zote upate haki zako. Ili kujisajili unatakiwa kuwa pesa tu ya ada kisha utapewa cheti cha uanachama, tayari vyombo hivi vitakuwa vimekutambua,” amesema Gunze.

 

Leave A Reply