The House of Favourite Newspapers

Hadithi Lab na TBL wazindua bando la kicheko.

0
Mwanzilishi wa Taasisi ya Hadithi Lab, Edward Shilla (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa “Bando la Kicheko” ambayo ni Ucheshi Wima (Standup comedy) utakaowezesha wanavyuo kupata burudani ya ucheshi na kuvumbua vipaji kutoka kwenye vyuo mbalimbali nchini. Wengine kulia ni Meneja Masuala Endelevu TBL Plc, Abigail Mutaboyerwa na Meneja Ubunifu na Uzalishaji wa Hadithi Lab, Tunu Mwinyimbegu.

Ni jukwaa la Vijana linalotumia sanaa ya uchekeshaji kuelimisha wanavyuo Disemba 10, 20202 – Dar es Salaam: Kampuni ya Hadithi Lab kwa kushirikiana na Tanzania Breweries Limited (TBL) leo wamezindua tamasha jipya la Bando Kicheko University edition; Kijanja. Bando la Kicheko ni jukwaa la vijana lenye kutumia sanaa ya uchekeshaji kuelimisha Vijana kupitia sanaa hiyo.

Dhumuni la kuandaa tamasha hili ni kwanza kuonyesha wanafunzi na Watanzania kwa ujumla burudani ya tofauti katika tasnia hii inayokua. Pili ni kuwapa burudani wanafunzi katika kipindi ambacho wanakuwa na sonona (stress).
“Tunaamini kuna nguvu katika Kicheko. Tunaamini mwanafunzi mwenye furaha ni mwanafunzi mwenye afya nzuri ya akili na tatu ni kuvumbua na kuonyesha vipaji vingi vya Sanaa ya uchekeshaji kupitia matamasha haya. Ambapo utaona kwamba baadhi ya wachekeshaji na waandaji wa matamasha haya ni wanafunzi wa tasnia ya Sanaa,” alisema Mkurugenzi wa Hadithi Lab, Edward Shila.

Kwa upande wake, mdhamini wa jukwaa hilo kutoka TBL, Abigail Mutaboyerwa alisema kwamba wanaamini kwamba kupitia uchekeshaji wataweza kusaidia kujenga taifa la vijana wenye furaha zaidi na wenye kujielewa.
“Sisi kama TBL tunatambua umuhimu wa kuwaburudisha wanafunzi kwa Sanaa ya tofauti lakini pia umuhimu wa kutumia pombe kistaarabu katika kipindi ambacho wanaanza kujitegemea na kujifunza mambo mapya,” alisema Mutaboyerwa

Meneja Masuala Endelevu TBL Plc, Abigail Mutaboyerwa akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa “Bando la Kicheko” ambayo ni Ucheshi Wima (Standup comedy) utakaowezesha wanavyuo kupata burudani ya ucheshi na kuvumbua vipaji kutoka kwenye vyuo mbalimbali nchini.

 

Matamasha haya yatafanyika katika mikoa 4, ambayo ni Dar es Salaam, Mwanza, Arusha and Dodoma ambapo katika tamasha hili la Sanaa ya uchekeshaji au stand up comedy vyuo vilivyoko katika mikoa tajwa vitashirikishwa kuandaa matamasha haya.

Bando la Kicheko ni Jukwaa la vijana lenye kufanya Sanaa ya uchekeshaji. Jukwaa hili lililoanzia Arusha limeundwa na Wasanii chipukizi 5 ambao waliungana kuonyesha vipaji vyao na kuwapa nafasi vijana wengine pia waweze kuonekana huku wakitoa elimu ya namna ya kuishi kijanja wakati wakiwa vyuoni.

 

 

Leave A Reply