The House of Favourite Newspapers

Halotel Yasherekea Siku ya Mwanamke Duniani Kivingine

0
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano Halotel Sakina Makabu akiongea na waandishi wa habari leo katika shule ya Sekondari Kisarawe II iliyoko wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel ikiwa ni sehemu ya jamii ya Tanzania inaendelea kujali na kuchangia katika maendeleo ya nchi kupitia nyanja mbalimbali.

Mbali na huduma ya mawasiliano ya simu, Kampuni imekuwa pia ikichangia maendeleo katika sekta ya huduma za jamii kama vile afya na elimu.

Akiongea na waandishi wa Habari leo wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika shule hiyo Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Sakina Makabu, amesema Tukiwa tunaelekea kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Halotel imeona ni muhimu kuadhimisha siku hiyo kwa kuchangia katika sekta ya elimu katika kusaidia juhudi za Serikali za kuendeleza sekta hiyo kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano Halotel Sakina Makabu (katikati kushoto) na Afisa Mahusiano Stella Pius (wa tatu kulia) wakikabidhi moja ya vifaa kwa Mkuu wa shule ya sekondari Kisarawe II Bw. Florentin Assenga kama ishara ya vifaa mbali mbali vya ujenzi kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo kwenye Bweni la Wasichana kidato cha tano na ikiwa ni moja ya msaada kutoka kampuni hiyo. 

Kupitia sera yake ya kurudisha sehemu ya faida kwa jamii (CSR), kampuni imechangia vifaa vya shule kwa shule ya sekondari ya Kisarawe II (A-level) iliyoko wilayani Kigamboni, ikiwa ni kuendana na kusherehekea Siku ya Wanawake duniani.

 

Kutokana na uhitaji wa shule hiyo, Halotel imechangia vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo kwenye Bweni la Wasichana kidato cha tano na sita.

Vifaa hivyo ni pamoja na tanki la Maji la lita 5000, Masinki ya kunawia mikono 4 (complete), malumalu (tiles) za ukutani na sakafu boksi 100, saruji mifuko 30, mchanga lori moja,na vinginevyo.

Wakiwa katika picha ya pamoja.

 

Sisi kampuni ya Halotel tunaamini kuwa vifaa hivyo ni muhimu katika kujenga na kuboresha mazingira ya shule ya kusoma na kujifunzia, na hasa kwa ajili ya usafi wa wanafunzi wa kike ili waweze kujisikia vizuri pindi wawapo shuleni na kuweza kupata masomo kwa ufasaha bila kuwa na changamoto. Alisema Sakina.

 

“Manufaa ya vifaa hivyo tunatarajia kwanza wanafunzi hao wa kike watakuwa na mazingira ya usafi rafiki wakati wote wanapokuwa shuleni hapo hivyo afya zao kuwa salama, itawawezesha kuwa na utulivu na kuweza kupata masomo kwa makini kitendo ambacho kinaweza kuongeza ufaulu wao binafsi, kwa shule, katika wilaya kimkoa na hata kitaifa”. Aliongeza Sakina.

 

Hii inaendana na kauli mbiu ya Siku ya Mwanamke mwaka huu ambayo inasisitiza katika kuleta usawa wa kijinsia leo kwa manufaa ya kesho.

Swala la usawa wa kijinsia, kama vile katika upatikanaji wa elimu, imekuwa ni mjadala duniani kote kwa muda mrefu sasa na uelewa wa swala hili umekuwa ukiongezeka miongoni mwa watu.

Uamuzi wa kampuni pia ni katika kuunga mkono juhuzi za Serikali katika kuboresha mazingira ya watoto wa kike kupata elimu bila vikwazo.

Kwa upande wake Afisa Tawala Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bi Pendo Mahalu alisema, “Tumefarijika sana kwa kupokea msaada huu kutoka Kampuni ya simu ya Halotel, tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa karibu na jamii na kuthamini lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kuisaidia sekta ya elimu nchini. Ninaamini kabisa vifaa hivi vitawasaidia wanafunzi wa kike walioko kidato cha tano na sita katika kuboresha mazingira yao kiafya na kuongeza ufanisi katika kupata elimu kwa ujumla”.

Sera ya kampuni kuhusu CSR ni kwamba hatuko tu kwa ajili ya kufanya biashara bali pia kujali na kurudisha kwa jamii kile tunachokipata ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha maisha na hali za watanzania katika sekta mbalimbali, na tumejikita hasa katika kuunga mkono juhudi za kuinua Elimu hasa kwa mwaka huu.

Leave A Reply