The House of Favourite Newspapers

Halotel Yatoa Mil. 50, Kuunga Mkono Juhudi za Makonda

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo.
Mhe. Makonda akipaua moja ya nyumba hizo za shule.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akipokea Hundi ya Milioni 50 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Halotel, Mhina Semwenda.
...Akishuka juu ya paa la ujenzi huo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapinduzi wakishiriki katika hafla hiyo.
Taswira ilivyoonekana katika hafla hiyo.

 

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel, imeunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kutoa kiasi cha shilingi Milioni 50 katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402 kati ya hizo shule 295 ni za elimu ya awali/msingi na shule 107 ni za sekondari zilizoko mkoa wa Dar es Salaam.

 

Akizungumza leo katika hafla ya uzinduzi wa ofisi ya walimu wa Shule ya Msingi Mapinduzi iliyopo Kigogo jijini Dar, Mhe. Makonda amesema wanaonunua maeneo ya shule hovyo wanatakiwa kukamatwa ambapo mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Shohan tayari amekamatwa kwa kununua sehemu ya eneo la Shule ya Msingi Mapinduzi.
“Angalau sasa napata usingizi kuona ndoto yangu inanitimia ya kuwapa ofisi nzuri za walimu,” alisema Mhe. Makonda.

 

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Halotel, Mhina Semwenda alisema kuwa;
“Hii ni moja ya sehemu ya jitihada zetu kama mtandao wa simu kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa, Makonda. Tunayo miradi mingi ya elimu tunayoifanya ikiwemo ya Internet kwa shule zaidi ya 400 Tanzania nzima pia tunashirikiana na Chuo Kikuu Cha Dar es Saalam kuhakikisha wanafunzi wanasoma kupitia mfumo wa Tehama.”

 

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo amemshukuru Makonda kwa jitihada zake anazozifanya katka mkoa huo kwa kuwaangalia walimu na kuweza kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuwawezesha kufanya kazi zao katika sehemu nzuri.

Comments are closed.