The House of Favourite Newspapers

Hamisa Mobeto Afunguka Kumzalia Watoto Watano Diamond

0

Wakati ndoa ya staa mkubwa wa muziki barani afrika, Nasibu abdul ‘Diamond Platnumz’ ikinukia, habari mpya ni kwamba mzazi mwenzake, mwanamitindo Hamisa Mobeto, amefunguka kuwa haoni tatizo kumzalia staa huyo mtoto wa tano, Gazeti la IJUMaa linakushushia mchapo kama wote!

ISHU IMEaNZIa INSTAGRAM

Mchongo huu ulianzia kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram ambako kulizagaa tetesi kuwa bwana Nasibu a.k.a Mondi ameshafanya yake kwa Mobeto na ujauzito ukitajwa kuwa na umri wa miezi mitatu.

“Wabongo wanasema bora mtu akunyime chakula, lakini siyo umbeya, kwa taarifa za sasa hivi unaambiwa mambo yameshataradadi huko kwa Mobeto na Chibu (Nasibu) ameshaweka chata nyingine kwa bidada hapa tulipo Dyllan anasubiria mdogo wake…

WAUNGANISHA DOTI…

“Tulikuwa tunajiuliza Hamisa (Mobeto) mbona amechachamaa na Mondi hivi kwenye kumvalisha kumbe mambo ni moto na unaambiwa siku hizi analala kwa Mondi. Ila kinachotushangaza wajameni bibie alisema hawezi kuzaa mtoto mwingine bila ndoa, sasa hatujui imekuwaje,’’ alifunguka mdau mmoja mwenye ushawishi Instagram.

WENGINE WAKAENDA MBALI

Kwenye Instagram, kuna wadau wengine walikwenda mbali zaidi kwa kudai ndiyo maana Mobeto hakuweza kuhudhuria kwenye sherehe ya harusi ya dada wa Diamond, Esma Khan ‘Esma Platinum’ iliyofanyika hivi karibuni kwa sababu Mondi ndiye aliyemzuia kwenda kwani mimba inampeleka puta.

 

“Wanazengo mnajua kwa nini bimdashi hakutokea kwenye shughuli ya Esma ambaye ni shoga yake wakati kwa Zuchu alikwenda? Unaambiwa mimba inampeleka hovyo anatematema mate mpaka mzee baba (Mondi) akamwambia atulie nyumbani asiende kwenye shughuli hiyo,” aliandika shabiki mwingine anayejiita Mrs–Muhidini.

MOBETO ANASEMAJE?

Ili kujua ukweli juu ya habari hizo Gazeti la IJUMAA lilifanya jitihada za kumpata Mobeto ambapo lilifika nyumbani kwake, Mbezi-Beach jijini Dar, lakini lilimkuta amelala na kushindwa kuzungumza naye ana kwa ana ila baadaye alipatikana kupitia simu ya mkononi.Mazungumzo kati yake (Mobeto) na Gazeti la IJUMAA yalikuwa hivi;

IJUMaa: Mambo

Hamisa,  mzima wewe?

MOBETO: Mimi mzima nani mwenzangu?IJUMaa: Unaongea na mwandishi wa Gazeti la IJUMAA.

MOBETO: Enhe, sema!

IJUMAA: Kuna habari zinasamba kwenye mitandao ya kijamii kuwa una ujauzito wa Mondi na ndiyo maana umekuwa karibu naye kwa kipindi hiki na umekuwa ukimvalisha nguo akiwa anatoka kwenye mambo yake, je, habari hizi zina ukweli kiasi gani?

MOBETO: (Anacheka) habari hizo nimeziona sana tu ila kwani mimi kuzaa na Mondi kwani ni ajabu mpaka watu watokwe mapovu kiasi hiki?(Maana yake haoni tatizo kumzalia jambo ambalo likifanyika, atamuongezea Mondi mtoto wa tano). “Unajua mimi sipendi watu wanifuatilie maisha yangu kabisa.

 

Na kuhusu kumvalisha Nasibu (Mondi), watu wafahamu kwamba mimi ni mfanyabiashara, natafuta pesa na siwezi kuchagua mtu wa kumvalisha eti kwa sababu ya kuogopa watu wa kwenye mitandao watasemaje, mimi sina shida yoyote na Nasibu (Mondi).

TUJIKUMBUSHE

Mondi na Mobeto walikuwa kwenye uhusiano wa siri wakati Mondi alipokuwa kwenye uhusiano wa wazi na bibie wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kufanikiwa kumzalia mtoto mmoja Dylan.

 

Zari aliposhtukia mchezo ndipo alipoandika waraka wa kumuacha Mondi kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Wapendanao (Valentine Day), Februari 14, 2018.

 

ANAWEZA KWELI KUZAA NA MONDI?

Kwa kuwa Mobeto mwenyewe haoni tatizo kuzaa naye, basi lolote linaweza kutokea na ikumbukwe siku za nyuma mrembo huyo alishawahi kukaririwa akisema kuwa, yeye atazaa hata watoto saba kama ikiwezekana kwa sababu kwao yupo mwenyewe.

Leave A Reply