The House of Favourite Newspapers

Hamza Johari: Anga la Tanzania Liko Salama

0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka  ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzisha kwa Mamlaka hiyo (wa kwanza kushoto ni Kushoto ni Tumaini Mgaya Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uongozaji Ndege,  Daniel Malanga, Mkurugenzi Udhibiti Uchumi na Kulia ni 
Rashid Khamis Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Usalama wa Usafiri wa Anga
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari amesema hakuna mlipuko wowote wa volcano utakaosababisha viwanja vya ndege vya Kilimanjaro na Arusha kufungwa, anga la Tanzania ni salama watu waendelee kuja.
Johari amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanza kusherekea kwa kuadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.
Amesema kuwa jana kuna taarifa zilisambaa kwamba viwanja hivyo vitafungwa kwa sababu kuna tishio la mlipuko kwenye Mlima Kilimanjaro, taarifa hizo sio sahihi kilichotokea kulikuwa na marekebisho ya umeme.
“Ukishatoa taarifa hizi za uongo mashirika ya Kimataifa yanaweza yakaogopa na watu wanaweza kuahirisha safari na kusababisha madhara makubwa, tumeanza kupigiwa simu na Ethiopia wakitaka ufafanuzi wa hili,” amesema Johari
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka  ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzisha kwa Mamlaka hiyo (wa kwanza kushoto ni Kushoto ni Tumaini Mgaya Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uongozaji Ndege,  Daniel Malanga, Mkurugenzi Udhibiti Uchumi na Kulia ni 
Rashid Khamis Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Usalama wa Usafiri wa Anga
Mkurugenzi huyo, amesema kilichotokea juzi katika uwanja wa Kilimanjaro ilipotoshwa kwamba hakuna umeme na ndege zimeshindwa kutua, taarifa hiyo sio sahihi, kinachoendelea ni maboresho ya ufungwaji wa taa kwa sababu ni za muda mrefu.
” Mareboresho haya yanafanywa kwa sababu taa za uwanja ni za muda mrefu. Kilichotokea wakati wanafanya majaribio nyaya zilipiga shoti taa zikazimika, lakini jenereta lilikuwepo, kwa hiyo hakuna tatizo ndege zinaendelea kutua,” amesema Johari
Aidha, amesema katika kusherekea miaka hiyo wamepata mafanikio makubwa katika uthibiti wa usalama katika sekta ya usafiri wa anga, mwaka 2003 walikuwa na marubani 234, lakini kwa sasa wapo 603.
Pia, amesema kwa kipindi kile kulikuwa na ndege 101 kwa sasa kuna ndege 206, kwa kipindi hicho idadi ya abiria kwa mwaka walikuwa milioni 1,521 hadi wanafunga mwaka 2022 abiria walikuwa milioni 5,723 ambalo ni ongezeko kubwa.
Johari amesema wanaendelea kunyambulika kwa sababu Serikali imewekeza sana kwenye sekta ya anga, mwaka 2003 waongozaji wa ndege (marubani wa chini) wanaotumia minara ya kuongoza ndege walikuwa 70 na kwa sasa wapo 154.
Pia, amesema mafanikio mengine ni kwa upande wa wahandisi wa mitambo ya kuongoza ndege umeongezeka mara mbili kutoka  20 ha 44, wataalam wa taarifa za anga wapo 83 kutoka 50, kwa ujumla idadi ya wataalam hao ni 281.
Amesema ili kuweza kulisimamia anga vizuri lazima kuwepo na mitambo ya Kisasa, kwa upande wa kuangazia walikuwa na rada moja ambayo ilikuwa inamolika kwa asilimia 25 kwa sasa wana rada nne zinamolika anga loye la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kwa upande wa uthibiti wa uchumi, kazi yetu ni kuhakikisha usafiri wa anga unakuwa endelevu na kuhakikisha unaendelea kukuwa na kuhakikisha tunatoa huduma nzuri abiria wafurahie,” amesema
Leave A Reply