The House of Favourite Newspapers

Hapatoshi Global FC vs Bongo Fleva

TIMU ya Global FC, keshokutwa Ijumaa inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Bongo Fleva FC kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe, Kibaha, Pwani.

 

Akizungumzia mchezo huo, Nahodha wa Bongo Fleva, Rich One, alisema maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya mchezo huo.

 

“Maandalizi yanakwenda vizuri ya mchezo wetu na kikosi chetu kina morali ya juu kuhakikisha tunapata ushindi.

“Kikosi chetu kinatarajiwa kuongozwa na wasanii wakubwa na maarufu ambao ni TID, Stamina,
Papii Kocha, M2 The P na wengine wengi,” alisema Rich One.

Kwa upande wa nahodha wa Global FC, Wilbert Molandi ‘Momo’ anayemudu kucheza nafasi ya kiungo, alisema kuwa: “Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kikubwa tunahitaji ushindi pekee.

“Tunatarajia kushusha mziki mzima katika mchezo huo kwa maana ya wachezaji wetu wote akiwemo Saleh Ally na Phillip Nkini.”

Comments are closed.