The House of Favourite Newspapers

Harmonize Kuvunja Rekodi ya WAAH ya Diamond? Attitude Yafikisha Views 3.4M

0

MSANII wa Bongo Fleva na C.E.O wa lebo ya Konde Gang Rajabu Abdul Kahali, maarufu Harmonize ambaye anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake wa Attitude aliowashirikisha wwanamuziki wa Kongo, Awilo Longombana na msanii wa muziki wa Bongo Bolingo, Hamis Ramadhani maarufu kwa jina la H. Baba anaifukuzia rekodi ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye aliiweka kupitia video ya wimbo wake Waah aliomshirikisha Mkongwe wa muziki Barani Afrika, Koffi Olomide.


Video hiyo ya Harmonize imepata watazamaji zaidi ya 3.4M You Tube chini ya masaa 48 akiifukuzia rekodi ya #Waah ya Diamond ambayo ilifikisha watazamaji 4.2M You Tube chini ya masaa 48. Harmonize amebaki na masaa machache kuifikia rekodi hiyo ya Diamond Platnumz

Leave A Reply