The House of Favourite Newspapers

Harris, Sinare Kuongoza Wajasiriamali Wanawake

0

Showbiz

WAZUNGUMZAJI wakubwa nchini, Harris Kapiga, Maza Sinare wanatarajiwa kuongoza semina kubwa ya wajasiriamali wanawake itakayofanyika Machi 13, mwaka huu katika Ukumbi wa Kamanyola-Sinza jijini Dar.
Akizungumza na Showbiz mratibu wa shughuli hiyo, Faith Victory Kivea alisema kuwa siku hiyo pia katika kutoa semina, watakuwepo wazungumzaji wengine ambao ni Mama Henjewele na Dk. Elie.

“Semina hii tumeipa jina la Mwanamke na Familia ambayo itakuwa maalum kuwasaidia wanawake katika kuinua uchumi, kumfanya mwanamke aweze kujikwamua kiuchumi na pia kumfanya kuwa msaada mkubwa katika familia na taifa kwa ujumla,” alisema Faith na kuongezea kuwa kiingilio kitakuwa shilingi 25,000.

Leave A Reply