The House of Favourite Newspapers

HARUSI YA MAFUFU: Steve Nyerere Amjaza Pesa Ukumbini! -Video

Msanii wa Bongo movies, Steve Nyerere akimjaza mapesa, Msanii wa filamu za Kibongo na Mwenyekiti Msaidizi wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Jimmy Mafufu wakati wa sherehe ya ndoa yake kwenye Ukumbi wa Alfa, Morocco jijini Dar, jana.
Steven Nyerere akichomoa pesa nyingine ili amtunze Jimmy Mafufu huku wasaidizi wa bibi harusi, Upendo wakikusanya pesa zilizodondoka chini.

Msanii wa Bongo movies, Steve Nyerere, jana amemfanyia kufuru msanii mwenziye wa filamu za Kibongo ambaye pia ni Mwenyekiti Msaidizi wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Jimmy Mafufu wakati wa sherehe ya ndoa yake kwenye Ukumbi wa Alfa, Morocco jijini Dar, baada ya kumjaza mapesa alipokwenda mbele kumtunza.

 

Steve baada ya kuitwa mbele alianza kwa kumpongeza Mafufu kwa kujitwalia jiko huku akimsihi amtunze mkewe na amheshimu ili ndoa yao iwe na amani na baada ya hapo alianza kumrushia pesa hizo.

PICHA/HABARI: BONIFACE NGUMIJE -GPL

Comments are closed.