The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Bobi Wine Apelekwa Marekani Kutibiwa – Video

MBUNGE wa Kyadondo nchini Uganda, ambaye inadaiwa aliteswa na maafisa wa usalama, Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina Bobi Wine tayari amesafirishwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi kutokana na maumivu na majeraha ya kipigo hicho.
Juzi, Alhamisi usiku Polisi walimkamata Bobi Wine na mbunge mwenzake wa upinzani Francis Zaake katika Uwanja wa Ndege wa Kampala wakati wakijiandaa kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu huku polisi wakidai kuwa viongozi hao wa upinzani, ambao wote wanakabiliwa na tuhuma za uhaini walikuwa katika harakati za kukimbia nchi.
Hata hivyo, wabunge hao wawili wamesema kuwa waliteswa baada ya kukamatwa huko nyuma na hospitali ya Kampala ilitoa pendekezo kwamba wapatiwe matibabu nje ya nchi.
Mwanasheria wa Haki za binadamu nchini humo Nicholas Opiyo kupitia twitter amesema ameshuhudia Wine akiondoka Uwanja wa Entebe kwa ndege ya KLM.

Comments are closed.