The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Yanga Wajinasua Algeria

0

ALGERIA: Hatimaye mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans ‘YANGA’ wamepata ndege ya kuwarudisha wachezaji wake nchini Tanzania kutokea nchini Algeria baada ya kuachwa na usafiri wao wa awali.

Hayo yamebainishwa na taarifa fupi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa akisema kwamba tayari wameshafanya utaratibu wakutafuta ndege nyingine ambapo wachezaji hao wanatarajiwa kuanza safari ya kurudi leo majira ya saa 10 kwa saa za Algeria.

 

“Tayari klabu imefanya utaratibu wakutafuta ndege nyingine hivyo msafara wa wachezaji waliokuwa wamekwama Algeria kwa kuachwa na ndege wataanza safari jioni ya leo majira ya saa 10 kwa saa za Algeria tayari kurejea nchini na tunatarajia kufika Tanzania mchana kesho siku ya Jumanne”. Alisema Boniface Mkwasa

Leave A Reply