The House of Favourite Newspapers

Davina Apagawishwa na Keki

0
Halima Yahya ‘Davina’ akiwa na wadau wa filamu Bongo.

DAR ES SALAAM: Mwigizaji wa kitambo Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ juzikati alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘birthday’ ambapo alijumuika na marafi ki zake kwenye Ukumbi wa Sparrows Launge uliopo Dar Free Market, Dar, lakini kilichowashangaza wengi ni jinsi alivyopata keki nyingi zilizompagawisha na kushindwa aanze kukata ipi.

Davina.

Davina aliliambia Wikienda kuwa, anawashukuru rafi ki zake wote waliompelekea keki ambazo zilikuwa nyingi hadi akashindwa aanze kukata ipi kwani zote zilikuwa muhimu.

“Nilianzia sherehe nyumbani. Nilikata keki na wanangu, lakini baadaye niliihamishia ukumbini, nikajumuika na mashabiki na baadhi ya rafi ki zangu,” alisema Davina.

 

Leave A Reply