The House of Favourite Newspapers

Hatua 10 za Kuchagua Mchumba Kuepuka Kashfa ya Kuwa na Wapenzi Wengi

0

WENGI wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake.

Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema, idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la wanaume/ mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na wapenzi wengi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa         mwanaume/ mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/ mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake.

Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake walewale wasio sahihi kwake.

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake.

Kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya tendo la ndoa na wanaume hao.

Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi?

Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa, wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huohuo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.

Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.

Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/ mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi.

Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji au muonjwaji, tabia ambayo huathiri mtu kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA- Ni mwanamke/ mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake.

Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha.

Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini?

Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa mioyo bure.

Itaendelea wiki ijayo, usikose!

EXCLUSIVE: SOPHIA wa ‘AMELOWA’ AFICHUA UKWELI PENZI LAKE na HARMONIZE, KUMLIZA KAJALA | DSM FLAVOUR

Leave A Reply