The House of Favourite Newspapers

 Hawa Ndio Majaji wa Public Speaking na Timu Zao

0

MAJAJI wa Shindano la National Public Speaking tayari wameshagawana washiriki 30 katika makundi matatu kwa ajili ya mafunzo yatakayotolewa kambini.

 

Shindano hilo ambalo linaitwa National Public Speaking lilizinduliwa Novemba 2019 ambapo lilianza na washiriki 300 ambao walipunguzwa hadi 170 kabla ya kufikia 80 na sasa ni washiriki 30 waliofanikiwa kuingia fainali kwenye shindano hilo.

 

ALICE GEORGE NCHWALI

Anafahamika zaidi kama Alice Prince, yeye ni muhamasishaji, mshauri na mjasiriamali. Jaji Alice anasema yeye ni mchapakazi, mchangamfu, jasiri na mwanadada mahiri lakini ni mke na pia mama.

 

Alice anaendelea kufunguka kuwa ana Shahada ya Uhasibu na pia amefuzu kiwango cha juu cha taaluma ya uhasibu nchini Tanzania (CPA (T)) na ni Mkurugenzi Mtendaji wa BMF Consult Limited ambayo ni kampuni inayotoa ushauri wa kihasibu, ukaguzi wa hesabu na kodi.

Alice anaamini washiriki wake wote kumi wapo vizuri na wanajiamini kutafuta ushindi.

 

Timu Alice ni hii hapa; Elikana Lihuwi, Mlebe Sadick, Nickson Everest, Lilian Proches, Eben Mzava, Baraka Konkara, Mastidia Gapi, Winnie Simplis, Chediel Wazoel na Goodluck Nkya.

 

RODRICK FREDRICK NABE

“Naitwa Rodrick Fredrick Nabe, ni mhamasishaji, muandaaji wa makongamano na mwandishi wa vitabu. Nafundisha pia makampuni na taasisi kuhusu maendeleo binafsi, malengo na namna ya kuongeza mauzo. Nina taaluma ya ualimu na sheria.

“Mimi ni mwanzilishi wa Road to Success Initiative, muasisi wa Investment Club na Mkurugenzi Mwenza wa Tanzania Institute of Public Speaking.

“Kuwepo kwenye National Public Speaking Competition kama jaji ni heshima kubwa ukizingatia kwamba hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu shindano la wazugumzaji linafanyika kwa nchi nzima. Nimekutana na vijana wenye nia na hamu ya kuelimisha jamii kupitia sana ya uneni,” anasema Nabe.

 

“Tujiandae kupokea wazungumzaji mahiri kutoka kwenye shindano hili. Global Group chini ya Mr Eric Shigongo imeweka historia kwenye tasnia ya uneni.”

 

Timu Rodrick ni hii hapa; Mikidadi Uhuru, Yonathan Kossam, Neema Mwanayo, Jesse Mbako, Mary Kiria, Meckson Lorden, Abdillahi Mpehe, Elvis Massawe, Anthonia Anthony na Hekima Mwakitalama.

 

MOSSES RAYMOND

Kwa jina lingine anaitwa kaka Samora, ni mshauri, mnenaji wa hadhara na mjasiriamali. Mosses ni mume wa Monalisa na baba wa Joshua, Joella na Josiah.

 

Mosses alianza kukusanya uzoefu katika ajira tangu mwaka 2002 mpaka 2015 ambapo alifanikiwa kuajiriwa sehemu mbalimbali kwenye sekta binafsi, serikalini, mashirika yasiyo ya kiserikali na kampuni za ushauri.

 

Kuanzia mwaka 2015 aliamua kustaafu mapema kwa hiari na kutoka kwenye ajira na kuingia kwenye shughuli binafsi kama mshauri (Consultant) maamuzi yaliyompa fursa ya kufanya shughuli nyingi za ushauri na makampuni ya ushauri (Consulting Firms ) zaidi ya kumi na kuhudumia makampuni na biashara mbalimbali ndogo, za kati na kubwa.

 

Kwa sasa Mosses ni sehemu ya kampuni zifuatazo Crystal Human Capital, MK Events, MR Solutions na Tanzania Institute of Public Speaking.

Mosses amebahatika kupata elimu ya juu kwenye masuala ya rasilimali watu, maendeleo, dini na falsafa.

 

“Kwanza ni heshima kubwa kuteuliwa na kufanya kazi karibu sana na Mwenyekiti wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo. Pili imekuwa ni fursa kubwa kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika tasnia ya unenaji nchini kwa kuibua vipaji vipya kabisa na kuongeza wanenaji mahiri hapa nchini,” anasema Mosses.

Timu Mosses; Heckman Maro, Ali Mfaume, Caroline Sigala, Deborah Lwilla, Charlotte Nzuki, Mossi Kilongosi, Joseph Raymond, Radhia Jambi, Laureen Bhoke na Aisa Foya.

MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

Leave A Reply