The House of Favourite Newspapers

Hawa Nd’o Watu 10 Matajiri Zaidi Kuwahi Kuishi Duniani

0

MWANZILISHI wa kampuni la  Amazon, Jeff Bezos, ndiye mtu tajiri zaidi duniani kwa sasa, kulingana na orodha ya jarida la Forbes la 2019 iliyotolewa wiki hii. Akiwa na mali yenye thamani ya $131bn (£99bn) ndiye mtu tajiri zaidi duniani.

 

Lakini yeye si mtu tajiri zaidi kuwahi kuishi duniani. Taji hilo linadaiwa kumilikiwa na Mansa Musa, mfalme wa karne ya 14 kutoka Afrika Magharibi ambaye utajiri wake ungeathiri uchumi wa taifa zima.

 

Akaunti zake zilikuwa na utajiri mkubwa, kitu ambacho kilikuwa vigumu kuweza kubaini thamani ya utajiri na uwezo wake, kulingana na Rudolph Butch profesa wa historia katika Chuo Kikuu cha California.

 

“Mansa Musa alikuwa tajiri zaidi ya mtu yeyote angeweza kuelezea”, Jacob Davidson aliandika kuhusu mfalme huyo wa Afrika katika tovuti ya Money.com mwaka 2015.

 

 

Mwaka 2012 Tovuti ya Marekani iliweka thamani yake kuwa $400bn, lakini wanahistoria wa kiuchumi wanakubaliana kwamba mali yake haikuweza kuhesabiwa kwa kutumia nambari.

 

Wakati huohuo, Gazeti la The Los Angeles Times liliripoti baada ya kifo cha Moammar Gadhafi kwamba alikuwa na zaidi ya dola bilioni 200 katika akaunti zake za benki, katika uwekezaji duniani.

 

Habari hiyo iliripotiwa mara kadhaa duniani huku baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kwamba Gadhafi alifariki akiwa tajiri zaidi ya watu watatu matajiri duniani, ambao ni Carlos Slim, Bill Gates and Warren Buffett – wakiunganishwa

Hiyo ni thamani kubwa ambayo ingemfanya kiongozi huyo wa zamani wa Libya kuwa mtu tajiri katika historia ya ulimwengu na pengine tajiri zaidi ya mtu yeyote tajiri kutoka Marekani aliyewahi kuishi isipokuwa Andrew Varnegie na John D Rockfeller.

Watu 10 matajiri zaidi kuwahi kuishi duniani.
Mansa Musa (1280-1337, Mfalme wa Mali ambaye mali yake haiwezi kuelezewa
Augustus Caesar (63 BC-14 AD, Mfalme wa Roma ) $4.6tn (£3.5tn)
Zhao Xu (1048-1085, Mfalme wa Shenzong of Song China) mali yake haikuweza kuhesabika
Akbar I (1542-1605, Mfalme wa Mughal India) mali yake haikuweza kuhesabika
Andrew Carnegie (1835-1919, Mfanyabiashara wa viwanda wa Uskochi na Marekani ) $372bn
John D Rockefeller (1839-1937) Mfanyabishara wa Marekani ) $341bn
Nikolai Alexandrovich Romanov (1868-1918, Tsar wa Russia) $300bn
Mir Osman Ali Khan ( 1886-1967, Ufalme wa India ) $230bn
William The Conqueror (1028-1087) $229.5bn
Muammar Gaddafi (1942-2011, -Mtawala wa Libya) $200bn

Chanzo: Money.com, thamani ya watu maarufu

Mfalme wa dhahabu

Mansa Musa alizaliwa 1280 katika familia ya watawala. Nduguye , Mansa Abu-Bakr, alitawala ufalm huo hadi 1312, wakati alipoamua kwenda safari.

Kulingana na mwanahistoria wa karne ya 14, Shibab al-Umari, Abu-Bakr alipendelea sana kuiona Bahari ya Atlantic na kile ilichokuwa nacho.

Aliripotiwa kuanza safari na msafara wa meli 2,000 na maelfu ya wanaume na wanawake pamoja na watumwa. Walienda na hawakurudi tena.

Wengine, kama vile mwanahistoria wa Marekani, Ivan Van Sertima, anadai kwamba waliwasili Marekani Kusini. Lakini hakuna ushahidi.

Ukweli ni kwamba Mansa Musa alirithi ufalme ulioachwa nyuma na nduguye. Chini ya uongozi wake ufalme wa Mali uliimarika kwa kiwango kikubwa.

 

Aliunganisha miji 24 ikiwemo Timbuktu.

Ufalme wake ulipanuka kwa takriban maili 2000 kutoka Bahari ya Atlantic hadi nchini Niger akichukua sehemu ambazo ndizo Senegal ya sasa, Mauritania, Mali, Burkina Faso, Niger, The Gambia, Guinea-Bissau na Ivory Coast.

Ardhi hizo zote zilikuwa na mali asili kama vile dhahabu na chumvi.

Wakati wa utawala wa Mansa Musa, ufalme wa Mali ulikuwa ukimiliki takriban nusu ya dhahabu zote duniani, kulingana na kumbukumbu ya Uingereza.

Na mali yote hiyo ilimilikiwa na mfalme huyo. Kama kiongozi, Mansa Musa alikuwa na uwezo wa kufikia utajiri wa kiwango chochote kile duniani, Kulingana na Kathleen Bickford, ambaye ni mtaalam wa sanaa ya Afrika katika Chuo Kikuu cha NorthWestern.

Vituo vikuu vya kibiashara ambavyo vilikuwa vikifanya biashara ya dhahabu na bidhaa nyingine vilikuwa chini ya himaya yake na alijipatia mali nyingi kupitia biashara hiyo, aliongeza.

Safari ya kuelekea Mecca

Japokuwa mfalme huyo wa Mali alikuwa akimiliki dhahabu nyingi, ufalme wake haukujulikana sana.   Hatua hiyo ilibadilika wakati Mansa Musa ambaye alikuwa Muislamu aliamua kwenda Mecca kuhiji akipitia jangwa la Sahara na Misri.

 

Mfalme huyo aliripotiwa kuondoka Mali na msafara wa watu 60,000. Alibeba ufalme wake wote na maafisa wake, wanajeshi, watumbuizaji, madereva wa ngamia na watumwa 12,000 mbali na idadi kubwa ya mbuzi, kondoo na chakula.

 

Ulikuwa mji uliokuwa ukipitia katika jangwa.

Mji huo na wakazi wake hadi watumwa wake walikuwa wamevalia dhahabu na nguo za hariri. Kulikuwa na ngamia 100 ambapo kila mmojawao alikuwa akibeba mamia ya pauni za dhahabu. Utajiri huo ulionekana zaidi wakati msafara huo ulipowasili mjini Cairo ambapo.

 

Mvuto wa dhahabu mjini Cairo

Mansa Musa aliacha hisia za kukumbukwa mjini Cairo, kwani hali ya kwamba al-Umar ambaye aliutembelea mji huo baada ya miaka 12  ya mfalme huyo wa Mali anakumbuka vile watu wa mji huo walivyomsifu mfalme huyo.

 

Aliwapatia watu dhahabu hali ya kwamba miezi yake mitatu mjini humo ilisababisha bei ya dhahabu kushuka thamani kwa kipindi cha miaka 10 hatua iliyoharibu uchumi.

 

Kampuni ya kiteknolojia ya Marekani SmartAsset.com inakadiria kwamba kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu, Hija ya Mansa Musa ilisababisha hasara ya $1.5bn (£1.1bn) katika uchumi wa eneo la Mashariki ya Kati.

 

Alipokuwa akirudi nyumbani, Mansa Musa alipitia tena Misri na kulingana na watu wachache akajaribu kusaidia uchumi wa taifa hilo kwa kuondoa dhahabu iliyokuwepo kupitia kuiomba kwa kiwango cha juu kutoka kwa wafanyabiashara wa Misri.

 

Wengine wanasema kuwa aligharamika sana hadi dhahabu alizokuwa nazo zikaisha. Lucy Duran wa Shule ya African and Oriental Studies mjini London anasema kwamba wanahistoria wa Mali walikasirishwa naye.

 

”Alitoa dhahabu nyingi ya Mali hali ambayo iliwafanya wanahistoria hao kutomsifu katika nyimbo zao na hadithi kwa kuwa wanaona kwamba alipoteza mali nyingi ya taifa hilo nje ya ufalme wake,” alisema.

 

Alipendelea sana Elimu

Hakuna shaka kwamba Mansa Musa alitumia ama kupoteza dhahabu nyingi wakati wa hija yake. Lakini ni kutokana na ukarimu wake wa kupitia kiasi ambapo alipata umaarufu duniani. Mansa Musa aliiweka Mali na yeye mwenyewe katika ramani kisawasawa.

Katika ramani ya Catalan Atlas kutoka mwaka 1375 , mchoro wa mfalme wa Afrika unaonekana umekalia ufamle wa dhahabu juu ya Timbuktu, akiwa ameshikilia kipande cha dhahabu mkononi. Timbuktu ilikuwa eneo maarufu barani Afrika na watu walitoka maeneo ya mbali ili kujionea eneo hilo.

 

Historia huandikwa na wageni, kulingana na waziri mkuu wa vita vya dunia vya pili nchini Uingereza Winston Churchil. Baada ya Mansa Musa kufariki 1337 akiwa na umri wa miaka 57, ufalme huo ulirithiwa na wanawe wa kiume ambao walishindwa kuuleta pamoja.

 

Mataifa hayo madogo yalivunjika na ufalme ukaisha. Kuwasili kwa Wazungu katika eneo hilo ndiko kulipiga msumari wa mwisho kwa ufalme huo. Iwapo wazungu hao wangewasili mapema wakati wa utawala wa Musa huku Mali ikisifika kwa jeshi lake kubwa na uwezo, mambo pengine yangebadilika.

Leave A Reply