The House of Favourite Newspapers

Haya Hapa Malengo Saba ya Mpango Wa Maendeleo Ya Taifa

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo leo amewasilisha bungeni mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2024/2025.

Mkumbo amesema malengo ya jumla ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa
wa mwaka 2024/2025 yako saba kama ifuatavyo:
1. Kuendelea kulinda mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa
Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano iliyopita.

2. Kuendelea na juhudi za kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula nchini kwa kuendelea kuongeza matumizi ya mbolea, mbegu bora na kilimo cha umwagiliaji.

3. Kuongeza uzalishaji na uuzaji wa bidhaa (pamoja na huduma) nje ya
nchi kupitia sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu na madini.

4. Kuweka mkazo wa pekee katika kuongeza thamani katika mazao
yanayozalishwa kupitia sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu na madini

5. Kuendelea kuongeza, kuboresha na kuimarisha ubora wa huduma za
jamii, ikiwa ni pamoja na elimu, afya, maji na umeme.

6. Kuendelea kupanua na kuimarisha miundombinu ya usafiri wa barabara,
reli, anga, na majini, na utunzaji endelevu wa mazingira.

7. Kujielekeza kwenye kufungua fursa katika sekta za madini ya kimkakati
(critical minerals), uvuvi wa bahari kuu (deep sea fishing), uchumi wa
kijani (green economy) na uchumi wa kidigitali (digital economy).

Leave A Reply