The House of Favourite Newspapers

Hazard Agoma Kuondoka Real Madrid, Apania Kuonesha Thamani Yake Kombe la Dunia

0
Nyota wa Real Madrid Eden Hazard amesema hafikirii kuondoka Santiago Bernabeu mwezi Januari

NYOTA wa zamani wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza anayekipiga na mabingwa wa Ulaya Real Madrod, Mbelgiji Eden Hazard amesema hafikirii nah ana mpango wa kuondoka Santiago Madrid mwezi januari labda kama klabu itaamua kumuondoa.

 

Gazeti maarufu la michezo nchini Hispania Marca limebainisha kuwa Hazard amedhamiria kuyatumia mashindano ya fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kama jukwaa la kuonesha ubora na thamani yake iliyomfanya ajiunge na miamba hiyo ya soka duniani akitokea klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza.

Eden Hazard alikuwa moja wa wachezaji bora duniani kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na miamba ya soka Duniani Real Madrid

“Sifikirii kuondoka Real Madrid dirisha dogo la usajili, nataka kuendelea kucheza ndani ya Real Madrid na nioneshe thamani yangu lakini kama klabu itaamua kuniondoka basi ntaondoka. Kwa sasa malengo yangu ni kufanya vizuri na timu yangu ya taifa kwenye mashindano ya fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.” amesema hazard

 

Tangu Hazard ajiunge na Real Madrid ameshindwa kuonesha thamani yake ndani ya kikosi hicho kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara huku Kocha Mkuu wa sasa wa klabu hiyo Don Carlo Ancelotti akishindwa kumtumia katika michezo yake licha ya kuwa sasa yupo fiti kucheza.

Leave A Reply