The House of Favourite Newspapers

Helikopta ya Jeshi Kenya Yapata Ajali

0

WANAJESHI kadhaa wa Jeshi la Ulinzi Kenya (KDF) wanahofiwa kupoteza maisha baada ya helikopta ya kijeshi kupata ajali katika Milima ya Ngongo katika Jimbo la Kajiado asubuhi ya leo.

 

Kamanda wa Kikosi cha Anga cha KDF, Meja Jenerali Francis Ogolla, amesema ajali hiyo imehusisha helikopta ya kijeshi, Mi 171e iliyokuwa katika safari ya mafunzo ya kijeshi na kueleza kwamba wanajeshi kadhaa wameokolewa na kukimbizwa jijini Nairobi kwa matibabu.

 

Kwa mujibu wa Ogolla, helikopta hiyo iliondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Moi majira ya saa mbili na dakika kumi asubuhi na kupata ajali dakika kadhaa baadaye na kulipuka.

Leave A Reply