The House of Favourite Newspapers

HEMED ADAIWA KUWA KIWEMBE BONGO MUVI

Hemed Suleiman ‘PHD’

SIYO ajabu kuona watu wanavuka maji ya Bahari ya Hindi na kwenda kuufuata ubuyu wa visiwani Zanzibar ambao wengi wanaamini kuwa umetengenezwa kwa ustadi na kuwekwa viungo ipasavyo.

UBUYU WA HEMED

Ubuyu unaomung’unywa mjini ni wa mwigizaji machachari wa kiume Bongo Muvi, Hemed Suleiman ‘PHD’ ambaye anadaiwa kukumbwa na skendo ya kuwa kiwembe.

 

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya Bongo Muvi, Hemed anadaiwa kutembea na mastaa kibao wa tasnia hiyo kisha kuwabwaga na kuendelea na maisha yake bila kujali chochote. Vyanzo hivyo viliweka wazi kuwa, baadhi ya mastaa wanaamini kuwa mwigizaji huyo anaringa, lakini ni mtanashati hivyo wakiwa wanajipendekeza kwake anachofanya ni kutembea nao kisha kutambaa mbele na kuwapotezea.

 

“Unajua wadada wengi wa Bongo Muvi, hasa mastaa wanampenda sana Hemed, lakini mara nyingi yeye anakuwa hana muda nao kabisa hivyo akiona wanamsumbua, anachofanya ni kutembea na staa kisha anambwaga wala hana muda wa kuendelea naye tena kwa sababu ana mwanamke ambaye amezaa naye na wanaishi wote,” kilisema moja ya vyanzo hivyo na kuongeza: “Sasa unaambiwa kuna mastaa ukiwatajia jina la Hemed hawana hamu naye kwa sababu walishatendwa na kuachwa solemba.”

 

HEMED ATIRIRIKA

Ijumaa Wikienda: Hemed mambo vipi? Kuna ubuyu au niseme madai mazito kuwa una tabia ya kutembea na mastaa wakubwa kisha unawabwaga na umepewa jina la kiwembe, je, ishu hii ikoje?

Hemed: Natembea nao kivipi? Yaani ninawataka mimi au?

Ijumaa Wikienda: Ndiyo tunasikia hivyo na ukishamaliza kutembea nao unatambaa…

Hemed: Mimi sijawahi kumtaka mtu Bongo Muvi labda wenyewe ndiyo wananitaka, lakini siyo mimi ninawatokea.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo kama wakikutaka wewe unawakubalia?

Hemed: Mimi kazi yangu ninabutua, nasepa zangu.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo hujaona wa kuwa naye ‘permanent’ pale Bongo Muvi?

Hemed: Hapana…mimi sina mpango wa kutoka na staa wa Bongo Muvi.

Ijumaa Wikienda: Mbona inasemekana wanakupenda mpaka wengine wanakutokea wenyewe na kukuambia wanakutaka?

Hemed: Ni kweli ila mimi si nina mtu wangu?

Ijumaa Wikienda: Vipi kuhusu mwanamke uliyezaa naye ndiye unatarajia kumuoa?

Hemed: Kuoa siwezi kusema kwa sasa, ila nimezaa naye.

Ijumaa Wikienda: Una watoto wangapi?

Hemed: Sita na kila mtoto ana mama yake.

Ijumaa Wikienda: Imekuwaje watoto sita kwa mpigo?

Hemed: Kati ya hao kuna mapacha, lakini pia wengine wanapishana miezi miwili hadi sita, mimi sioni tatizo cha msingi ni kujua malezi yao tu.

Ijumaa Wikienda: Unawezeje kuwahudumia na hivi sasa filamu zinayumba?

Hemed: Naweza kabisa na ndiyo maana hujaona hata mwanamke mmoja analalamika kwenye chombo chochote cha habari kuwa nimetelekeza mtoto.

Ijumaa Wikienda: Mara nyingi kwenye ukurasa wako wa Instagram unamuweka yule mtoto wako wa kiume tu, kwa nini huwaweki wengine?

Hemed: Ni kwa sababu ndiye niko naye karibu kila wakati, lakini wengine unakuta mama zao wanakataa.

Ijumaa Wikienda: Hemed huo ndiyo ubuyu unaoenea mjini nasi tunashukuru kwa kufunguka.

Hemed: Ndiyo uwaambie hivyo na karibu tena kwa ubuyu mwingine kama upo.

UBUYU WAHITIMISHWA

Kwa muda mrefu safu hii ilipokea ubuyu huo wa Hemed na umekuwa ukimung’unywa sana hivi karibuni hivyo mmemsikia mwenyewe alivyouhitimisha.

MAKALA: Imelda Mtema, DAR

Mama Mzazi wa Isaac Gamba: Sitomsahau Mwanangu

Comments are closed.