The House of Favourite Newspapers

SERIKALI YAFUNGIA KAZI BIDHAA FEKI!

DAR ES SALAAM: Serikali ya awamu ya tano kweli siyo mchezo! Hivyo ndivyo walisikika baadhi ya watu wakizungumza kutokana na maofisa wa Serikali kusambaa kila kona kufanya msako na ukaguzi wa bidhaa mbalimbali zinazotengezwa hapa nchini na zinazoingizwa kutoka nje ya nchi bila kufuata utaratibu na zilizoisha muda wake.   

 

Ijumaa iliyopita maofisa afya wa Manispaa ya Kinondoni walifungia kazi bidhaa feki ambapo wakiwa katika oparesheni hiyo walifika kwenye godauni moja lililopo Mbezi-Africana jijini Dar ikiwa ni baada ya kupata taarifa za siri kuwa ndani ya godauni hilo zilihifadhiwa bidhaa zilizokwisha muda wake ikiwemo tomato sosi, soda za kopo na bidhaa nyingine.

Wakati maofisa hao wakiingia kwenye godauni hilo, kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers nacho kilitonywa juu ya taarifa hizo ambapo kiliwahi eneo la tukio na kukuta maofisa hao wakiendelea na ukaguzi wao. Wakaguzi hao wakiwa na wanasheria walionekana wakilikagua godauni hilo, lakini kwa bahati nzuri walikuta bidhaa zote zilizokuwemo zilikuwa hazina matatizo.

 

Bidhaa zilizokutwa ni soda zilizosindikwa kwenye makopo na tomato sosi, vyote kutoka nje ya nchi, lakini vyote vilibainika kuingia nchini kihalali na vilikuwa bado havijamaliza muda wake. Katika kujiridhisha, maofisa hao waliomba wafunguliwe na makontena yaliyokuwa nje ya godauni hilo ambayo nayo yalifunguliwa na kukutwa hayana bidhaa yoyote.

Baada ya kuyakagua makontena hayo na kuambulia patupu waliyageukia malori ya kampuni hiyo ambayo nayo waliyakagua na kukuta hayana mzigo wowote uliokuwa kinyume cha sheria hivyo maofisa hao baada ya kujiridhisha waliendelea sehemu nyingine.

 

Hivi karibuni imeibuka tabia ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiuza kiujanja bidhaa zilizoisha muda wake wa matumizi hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi wanaotumia bidhaa hizo.

STORI: RICHARD BUKOS, Wikienda

Mama Mzazi wa Isaac Gamba: Sitomsahau Mwanangu

Comments are closed.