The House of Favourite Newspapers

Henderson Ala Shavu Man U, Kumuweka Nje De Gea

0

KUNA uwezekano kipa namba mbili wa Manchester United, Dean Henderson, akamuweka benchi kipa namba moja wa kikosi hicho, David de Gea kwenye mchezo dhidi ya Newacastle.

 

Leo Jumapili, Man United itakuwa mwenyeji wa Newcastle kwenye Dimba la Old Trafford katika mchezo wa Premier League.

Henderson alidaka mechi iliyopita ya Europa League wakati Man United ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Real Sociedad.Kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer alisema: “Dean yuko vizuri, akiwa golini anapiga kelele, hilo linamsaidia kwa kiasi kikubwa, amekuwa vizuri ana uwezo wa kupambana na kuisaidia timu.

 

“Lakini siwezi kusema David sio kipa mzuri, ni kipa wangu namba moja, amekuwa akituokoa mara nyingi kama ile mechi na West Brom, alitubeba sana.“Kitu kingine ni kwamba kama nataka kufanya mabadiliko siku zote naongea na wachezaji wangu kwanza tunapanga nini cha kufanya, hivyo anaweza kuwa De Gea au Dean, lakini wote wanaisaidia timu

Leave A Reply