Henock Ampa Jeuri Gomes

KOCHA Mkuu wa Simba raia wa Ufaransa, Didier Gomes ameonekana kuvutiwa na kiwango cha Mkongomani, Henock Inonga Baka. Henock ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo msimu huu katika kukiimarisha kikosi chao.

Mmoja wa mabosi wa Benchi la Ufundi la Simba, ameliambia Spoti Xtra, Gomes amevutiwa na kiwango cha nyota huyo kutokana kumudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji namba 6 na beki wa kati 4 na 5.

Bosi huyo alisema kuwa Gomes jana asubuhi alimrejesha kucheza namba 5 inayochezwa na Joash Onyango, Pascal katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Cambiaso Academy uliochezwa Uwanja wa Boko, Dar ambapo alifanikiwa kufunga bao moja katika sare ya 1-1.

Alisema Gomes katika michezo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji na Biashara United, alikuwa akimchezesha namba 6 baada ya Sadio Kanoute kupata majeraha.

“Gomes anapenda mchezaji anayemudu kucheza nafasi zaidi ya moja katika timu yake kwa maana ya kiraka, hivyo ujio wa Baka umeonekana kuwa na faida kwake.

“Baka ana faida mbili za kucheza nafasi zote za beki wa kati na kiungo mkabaji, katika michezo hii miwili ya kirafiki tuliyocheza dhidi ya Cambiaso, Gomes alimtumia kucheza namba 5 na ameonekana kucheza vizuri pamoja na Nyoni (Erasto),” alisema bosi huyo.

~~WILBERT MOLANDI, Dar2179
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment