The House of Favourite Newspapers

Henock Baka Amtaja Mugalu

0

BEKI mpya wa Simba, Henock Inonga Baka amesema kuwa Chris Mugalu ndiye mchezaji ambaye anampa ushirikiano mkubwa katika kuyazoea kwa haraka maisha yake ndani ya Simba.

 

Baka ambaye ni beki wa Kati, amesajiliwa na Simba akitokea katika Klabu ya DC Motema Pembe ya nchini DR Congo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Baka alisema kuwa Mugalu amekuwa akimpa ushirikiano mkubwa wa kuhakikisha kuwa anayazoea mazingira mapya ndani ya Simba pamoja na kumfundisha jinsi ya kuongea Kiswahili.

 

“Mimi na Mugalu ni marafiki tangia zamani, nimefurahi kumkuta hapa ndani ya Simba yeye ndiye anafundisha kila kitu kuhusu Simba na kuzungumza kiswahili hivyo nashukuru kwa hilo, alisema Baka.

 

Simba mara baada ya kukamilisha usajili wa beki huyo sasa watakuwa na mabeki wa kati watano ambao ni Pascal Wawa, Etasto Nyoni, Joash Onyango na Kennedy Juma.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave A Reply