The House of Favourite Newspapers

Hesabu Kuibeba Simba CAF, Yapigwa na JS Saoura 2-0

MAKOSA ya safu ya ulinzi ya Simba, jana yaliigharimu timu hiyo na kujikuta ikipigwa mabao 2-0 na JS Saoura nchini Algeria lakini wamesisitiza kwamba nguvu zote sasa ni kwa AS Vita Jumamosi. Simba sasa imeelekeza nguvu zote kwenye mechi ya AS Vita ili kucheza karata ya mwisho ya kutafuta nafasi ya kufuzu robo fainali. Hesabu zinaibeba Simba kwani ikishinda mchezo huo itafi kisha pointi tisa na kusonga mbele.

 

Kwenye mechi ya jana safu ya ulinzi ya Simba chini ya Paschal Wawa, Mohammed Tshabalala na Paul Bukaba
haikuwa na uelewano mzuri jambo ambalo liliwapa Saoura nguvu ya kushambulia.

Mabao ya wenyeji yalifungwa na Yahya Sherrif kwa shuti la kiufundi huku la pili likipachikwa na Mohammed Amine kwa penalty. Amine alifanyiwa faulo na Bukaba ambaye kipindi cha kwanza nusura ajifunge alipokuwa akiokoa.

 

Sasa Simba imeelekeza nguvu zake kwa mechi ya Jumamosi saa moja usiku kwenye Uwanja wa Taifa ambayo
wamesisitiza kwamba hata kama Mwinyi Zahera wa Yanga atauza siri zao kwa Vita potelea mbali lakini ushindi lazima.

 

Kocha wa Simba,Patrick Aussems amefunga ukurasa wa mchezo wa jana na kuanzia leo ni kazi moja tu huku mashabiki nao wakisisitiza kupambana. Zahera aliliambia Spoti Xtra kwamba; “Simba atamfunga Vita kwenye Uwanja wa Taifa na wanaweza kwenda robo  fainali, lakini haiwezi kubeba ubingwa wa Afrika.”

 

“Haina timu yenye uwezo huo. Lakini ni ukweli usiofi chika kwamba mimi Vita nitawapa mbinu za Simba kwavile wale ni rafi ki zangu na kocha wao ni bosi wangu kwenye timu ya Taifa. “Siwezi kuwafi cha, ila itakuwa ni mechi ngumu sana na nzuri,”alisema Zahera ambaye anadai kwamba Simba inamuombea mabaya kwenye Ligi Kuu na FA.

Comments are closed.