The House of Favourite Newspapers

HII NDIYO COLLABO YA KANYE WEST, AMIGOS

0

MSANII wa muziki wa HipHop kutoka Marekani, Kanye West, amefunguka kuhusu ujio wa collabo yao inayotaka kuja hivi karibuni baada kuonekana wakiwa na msanii wa HipHop kutoka Marekani anayefahamika kama Amigos kwenye maeneo ya studio yake huko Calabasas.

Tetesi za collabo kati ya Amigos na Rapa Kanye West zimesambaa baada ya Quavo na Kanye West kuonekana pamoja katika studio ya Kanye West huko Calabasas.

Wasanii wachache wanaopenda mashabiki zao wajue kuwa kuna collabo inakuja na msanii fulani lakini imekuwa tofauti kwa wasanii wa nchi zingine kwani wamekuwa watu wa kimya sana pale ambapo wanataka kufanya collabo au kama wameshafanya wanakuwa kimya.

Katika nchi kama Tanzania au Afrika inatakiwa wasanii wasitangaze collabo zao ili wawashtukize mashabiki wawe na hamasa pale wanapotaka kutoka nyimbo zao ili wauze kama wasanii wa nje.

NA : SAMSON JEREMIAH

Leave A Reply