HII NI AIBU NZITO KIGOGO MATATANI KWA MKE WA MTU

DAR ES SALAAM: Ukiambiwa mke wa mtu sumu na ukaendelea kubisha yatakufika mazito kama ambavyo kigogo wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Freddy Sifael Manogi alivyojikuta matatani, Uwazi lina habari kamili.

 

Freddy ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Ngorongoro iliyopo Arusha, amefikishwa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akilalamikiwa kutembea na mwanamke aliyejulikana kwa jina la Suzan ambaye ni mke wa mtu. Max Ramadhani, mkazi wa Bahari Beach jijini Dar, amemburuza Freddy kwenye tume hiyo kwa barua iliyojaa tuhuma nzito.

 

NI TANGU 2016?

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Max ambaye ni mfanyabiashara wa madini, amedai kuwa Manongi alianza kumfuatilia na kutembea na mkewe huyo tangu mwaka 2016 hadi sasa. “Nilibaini Manongi anatembea na mke wangu tangu mwaka 2016.

 

Baada ya kunasa ushahidi wa meseji zao, nilimbana mke wangu, akakiri kutembea naye, akaniomba radhi na kuahidi kutoendelea naye. “Baada ya kukiri na kuahidi kutorudia tena, nilimsamehe mke wangu lakini pia nilimuonya Manongi aache kutembea na mke wangu,” alidai.

ADAIWA KUENDELEA

Max alidai kuwa licha ya mkewe kuahidi kutoendelea na mahusiano na kigogo huyo wa Ngorongoro, baadaye inadaiwa walirudiana na kuendelea kujinafasi. “Unajua shughuli zangu mimi ni za kusafirisafiri mara kwa mara sasa huku nyuma nikawa naelezwa kwamba mke wangu anaendeleza mahusiano na Manongi.

 

AFANYA UCHUNGUZI

“Nikawa nafanya uchunguzi wangu tu kwa siri na nikajiridhisha tena kwamba ni kweli wanaendelea na mahusiano,” alidai Max.

 

AIBUKA KIMYAKIMYA

Akizidi kueleza mazingira ya kunasa ushahidi wa mkewe kuendelea na uhusiano na Manongi, Max alidai kuwa alifanikiwa baada ya kurejea nyumbani kwake Mei 3, mwaka huu bila kumtaarifu mkewe.

“Nilipofika nyumbani nilimkuta mke wangu ana simu mpya ndogo aina ya Samsung na kwa kuwa nazifahamu simu zake, nikaanza kuikagua hiyo simu mpya.

 

SIMU YAMPONZA KIGOGO

“Humo ndani nikakuta mawasiliano yao na meseji nyingi za kawaida pamoja na za WhatsApp. “Kwenye upande wa WhatsApp, meseji nyingi zilikuwa ni za kuitana mke na mume wangu (Manongi na mkewe). Wanawasiliana mara kwa mara, wakipeana ratiba za siku, kujuliana hali na wakati mwingine kupeana ahadi za lini wataonana maana wamemisiana,” alidai Max.

 

AZIDI KUTIRIRIKA

Akizidi kueleza sakata hilo kwa uchungu, Max alisema katika meseji hizo za WhatsApp, Manongi alionekana kumsihi mkewe mara kwa mara afute meseji zao wanazochati. “Mke wangu alikuwa akimuahidi kuzifuta lakini hata hivyo inaonekana hakuwa akifuta maana anajua fika hii simu pamoja na namba yake wanaitumia kuwasiliana wao tu hivyo si rahisi mimi kuijua,” alidai.

 

MESEJI ZA KAWAIDA BALAA

Akizungumza na Uwazi huku machozi yakimlengalenga, Max alidai kuwa alipopekua kwenye upande wa meseji za kawaida ndiko alikokuta balaa zaidi maana alikuwa hadi

meseji za kuelekezana hoteli wanayokwenda kufanya yao. “Yaani nimeumia, unaona kabisa meseji wameelekezana wakutane palepale wanapokutania, wakaelezana kabisa chumba namba 607. “Isitoshe baada ya kufanya waliyoyafanya, wanapongezana kwa kuelezana jinsi walivyoinjoi siku hiyo,” alidai Max.

 

UWAZI LAONESHWA USHAHIDI

Mbali na kusimuliwa tukio hilo, Max alilionesha Uwazi ushahidi huo wa meseji na kujionea kinachodaiwa kuwa ni mawasiliano ya kimahaba.

 

‘MANONGI’ YUPO MAKINI…

Kwenye meseji hizo, kuna meseji mbalimbali zinazodaiwa  zimetoka upande wa Manongi zikimtahadharisha mara kwa mara mke wa Max afute mawasiliano yao ili yasije kuonekana. Aidha meseji nyingine zilikuwa za kuomba kutumiana picha ambapo Uwazi liliziona huku nyingine zikiwa zimeambatanishwa na ‘viemoji’ vya kimahaba.

 

SEHEMU YA MESEJI ZILISOMEKA

“Utanisubiri pale juu Restaurant.” “Okay sawa mume wangu.” “Mhhhhhhhh!” “Nane na nusu sio?” Aidha Uwazi liliona pia mtiririko mwingine wa meseji wanaodaiwa kutumiana wawili hao, Alhamisi ya Aprili 25 mwaka huu, ambapo ulikuwa unasomeka hivi: “Mume wangu.” “Mke wangu, (akarudiwa tena kuandikwa), Suzan Freddy.” “Mume wangu kipenzi.” “Uko poa?”

 

MESEJI YAMTISHA MAX

Aidha mbali na meseji nyingi za kimahaba kuzikuta kwenye simu ya mke wake moja ndiyo iliyomuogopesha ambayo mtu anayedaiwa kuwa ni Manongi alimjibu Suzan “Afe jamaa” ili kiu ya wawili hao kuinjoi pamoja toka asubuhi hadi jioni itimie.

 

ACHUKUA HATUA

Baada ya kuona meseji hiyo yenye viashiria vibaya vya kutishia uhai wake, Max aliamua kwenda Kituo cha Polisi na Kimara Temboni kufungua jalada la uchunguzi lililosomeka KMT/RB/1471/2019 TAARIFA.

 

AMTUMIA UJUMBE MANONGI

Max alieleza kuwa, miongoni mwa hatua alizozichukua ni pamoja na kumueleza Manongi kuwa amefahamu kuwa bado anatembea na mke wake. Anasema licha ya kumueleza jambo hilo, kigogo huyo hakumjibu chochote zaidi ya kukaa kimya licha ya kumtumia baadhi ya meseji alizozinasa katika simu ya mkewe.

 

ATINGA TUME YA MAADILI

Max hakuishia hapo, aliamua kuiandikia barua Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo chini ya Ofisi ya Rais. Kwenye barua hiyo (sehemu ya barua hiyo pichani) aliyoiandika Mei 17, mwaka huu ambayo Uwazi linayo, Max alieleza kwa kina malalamiko yake hayo ya kuchukuliwa mkewe na Manongi ambaye ni mtumishi wa Umma.

 

Alieleza kuwa alimkanya Manongi zaidi ya mara nne lakini amekataa kufanya hivyo, ameendelea kumchukulia mkewe. Katika barua hiyo, Max aliambatanisha na ushahidi wote wa meseji na akawaeleza kwamba yupo tayari kutoa ushahidi zaidi pale atakapohitajika.

 

AJIBIWA

Siku chache baadaye, Mei 21 mwaka huu, Mkuu wa Kanda Maalum-Dar es Salaam kutoka Sekretarieti ya Maadili, Getrude Cyriacus alimjibu Max kupitia barua yenye kumbukumbu Na CLA.76/429/04.

 

Kwenye barua hiyo mkuu huyo wa kanda alikiri ofisi yake kupokea malalamiko yake na katika uchambuzi wa awali, imebainika mtuhumiwa anafanya kazi Ngorongoro ambayo ipo Kanda ya Kaskazini – Arusha hivyo shauri hilo limepelekwa kanda hiyo kwa ajili ya hatua zaidi kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na Uwazi mara baada ya kupokea barua hiyo ya sekretarieti, Max alisema anaipongeza idara hiyo ya serikali kwani wamechukua hatua haraka kushughulikia suala hilo na anaamini haki itatendeka ili mhusika aweze kukomeshwa tabia yake.

 

“Nimeshapigiwa simu na watu wa Arusha, wanazidi kulifanyia kazi suala langu, naamini hatua za kimaadili zitamkuta Manongi ili iwe fundisho hata kwa viongozi wengine wa Serikali ambao wanatumia nafasi zao za kazi kuwaonea wengine,” alisema Max.

 

MANONGI ANASEMAJE?

Uwazi lilijaribu kumpigia simu Manongi siku na saa tofauti lakini simu zake mbili ziliita muda mrefu bila kupokelewa. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi ulioeleza madai yote anayotuhumiwa na Max, hakujibu chochote hadi tunakwenda mitamboni.

 

SUZAN ATAFUTWA

Aidha, mwandishi wetualimtafuta mke wa Max iliazungumzie sakata hilo nayehakupatikana.
Toa comment