The House of Favourite Newspapers

MWILI WA DADA WA SHIGONGO WATOLEWA MOCHWARI MWANZA

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Vaileth James Bukumbi ukitolewa mochwari ya Hospitali ya Bugando kupelekwa nyumbani kwake Nyamhongolo jijini Mwanza.

MWILI wa dada wa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, marehemu Vaileth James Bukumbi, leo umetolewa katika mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza na kupelekwa nyumbani kwake Nyamhongolo jijini Mwanza ambapo  kesho utasafirishwa kupelekwa Bupandwamhela kwa ajili ya mazishi.

Ndugu wa marehemu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Global Group, Masha Bukumbi,  waliuaga mwili huo.

Mwili ukiingizwa garini kuelekea nyumbani kwa marehemu.
…Ukiwasili nyumbani.
Shigongo akiongea na ndugu na waombolizaji baada ya mwili kufikishwa nyumbani.
Mwili ukiwa ndani ya nyumba yake.
Ndugu na jamaa wakimwaga marehemu.
Masha akibubujikwa machozi baada ya kuuaga mwili wa mdogo wake.
Ndugu wa marehemu wakisubiri kuuchukua mwili Hospitali ya Bugando.

Picha zote na Johnson James

Comments are closed.