The House of Favourite Newspapers

HII NI ZAIDI YA OFA REJESHA CAMON, NYAKUA CAMON 11 MPYA KUTOKA TECNO 

TECNO kuwasogeza karibu watumiaji wa simu za TECNO camon na hii ni baada ya tetesi zinazoendelea mitandaoni kuwa watumiaji wa TECNO camon 11 watapata ofa ya kubadilishiwa simu zao za TECNO camon kwa camon 11 mpya.

TECNO camon 11 inasemekana huenda ikawa simu ya kwanza kufungua dimba la teknolojia mpya ya notch screen na camera yenye artificial intelligence katika simu za TECNO.

 

Na ukiachilia kwamba matoleo ya camon yanasifika zaidi katika upigaji picha kali, lakini pia inasemekana huenda camon 11 ikawa sio simu ya kuiangalia mara moja ukaridhika na hii ni kutokana na tetesi za wadau kwamba, camon 11 inawezekana ikawa na umbo pana na jembamba lenye kung’aa mithili ya maji yamulikwayo na jua kali.

 

Pia huenda camon 11 ikawa na kioo cha nchi 6.2HD+ au zaidi.

Lakini pia fununu kuhusiana na ubadilishwaji wa simu za camon inasemakana kuwalenga watumiaji wa TECNO camon cx, camon cx air, camon cm, camon x na camon xpro.

Comments are closed.