The House of Favourite Newspapers

LAVALAVA AFUNGUKA KUMTELEKEZA MWANAMKE

Abdul Iddi ‘Lava Lava’

HITMAKER wa Go Gaga kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Abdul Iddi ‘Lava Lava’ amefungukia tetesi za kuwa amemtelekeza mwanamke na mimba yake na kukanusha kuwa sio kweli ila anashukuru kwa Baraka ya kupewa mtoto hewa.  

 

Akizungumza na Za Motomoto News Lava Lava alisema uvumi huo hata yeye alisikia na kuona baadhi ya video ambazo zilivujishwa kama ushahidi juu ya uhusiano wake na mwanamke huyo akidai kuwa ana mimba yake, lakini hata hamfahamu.

 

“Niliwahi kutumiwa meseji nyingi na mojawapo ni ya mwanamke huyo ambaye yupo nyumbani tu hafanyi muziki ila alikuwa anataka kuwa staa tu, aliniambia anataka kufanya kiki na mimi awe staa nisimchukulie vibaya, nikaisoma na kuiacha,”alisema Lava Lava.

Lava Lava ni mmoja kati ya wasanii kutoka WCB watakaokinukisha katika shoo ya kwanza ya Wasafi Festival itakayofanyika Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Novemba 24, mwaka huu kwa kiingilio cha shilingi 10,000 tu.

 

Tamasha hilo litakuwa la kihistoria maana itahusisha wasanii wote kutoka katika Lebo ya Wasafi akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Mbosso, Queen Darleen pamoja na Rayvanny.

 

Wasanii wengine watakaopafomu katika jukwaa hilo ni pamoja na Young Killer, Chin Bees, Country Boy, Khadija Kopa, Stereo na Dully Sykes. Hao ni baadhi tu ya wasanii waliotajwa lakini listi bado inaendelea.

Stori; Shamuma Awadhi, Dar

LAVALAVA: “Diamond Ana Mapungufu / Tunavumilia / Alikiba…”

Comments are closed.