The House of Favourite Newspapers

Himid Mao: Yanga Leteni Mkwanja Nisaini

0

Musa Mateja na Wilbert Molandi | CHAMPIONI

KIUNGO mkabaji anayesifika kwa kucheza soka la nguvu, Himid Mao ‘Ninja’ ametamka kuwa kama ni kweli Yanga wanamhitaji, basi wamuwekee fedha mezani asaini.

Kauli hiyo, aliitoa kiungo huyo juzi Jumatano dakika chache mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea Misri alipokuwa kambini na Taifa Stars.

Himid amekuwa akitajwa kuwa anahitajika Yanga ili kuchukua nafasi ya Mzambia, Justine Zulu ambaye ameonekana kushindwa kuimudu nafasi hiyo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mao alisema yeye ni mchezaji huru hivi sasa anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote inayomhitaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Aliongeza kuwa anachokiangalia ni maslahi na kitu kingine huku akisubiria ripoti ya majaribio yake aliyokwenda kufanya Klabu ya Randers inayoshiriki Ligi Kuu ya Denmark.

“Mimi na wakala wangu hatujafuatwa kwa mazungumzo yoyote ya usajili. Nimekuwa nikisikia tu taarifa hizo za kuwaniwa na Yanga na Singida United.

Wao Yanga kama kweli wa nanihitaji, basi waje mezani tuzungumze kwa kumfuata wakala wangu,” alisema Mao.

Leave A Reply