The House of Favourite Newspapers

Historia Fupi ya Marehemu Vaileth Bukumbi, Dada wa Shigongo

Mtoto wa marehemu Vaileth, Deus James Bukumbi,  akisoma historia fupi ya marehemu.

 

MWILI wa dada wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, marehemu Vaileth James Bukumbi, unaagwa leo Ijumaa, Juni 21, 2019, nyumbani kwao katika Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosa – Sengerema mkoani Mwanza.

Askofu Peter Kitula akiongoza ibada ya kuaga mwili wa marehemu.

Historia fupi ya Vaileth Bukumbi

Vaileth alizaliwa mwaka 1979 na kumaliza elimu ya msingi  1992 ambapo alianza kujishughulisha na biashara mbalimbali.

Watoto wa marehemu wakiwa wenye huzuni.

Alibatizwa mwaka 1986, na  1995 alifanikiwa kupata mchumba akaolewa na kuzaa watoto sita,  wa kiume wawili na wa kike watatu.

Katika kujishughulisha kwake, Vaileth alifanikiwa kumiliki Kampuni ya Hamo Marine Transport iliyokuwa ikijishughulisha na huduma za usafirishaji.

Mbunge wa Magu, Boniventura Kiswata, akiomboleza msiba wa Vaileth.

Vaileth alianza kuugua mwaka 2014, akisumbuliwa na matatizo ya tumbo, alipelekwa nchini India akafanyiwa uchunguzi na kukutwa na tatizo la mfumo wa chakula.  Alitibiwa na afya ikaimarika akaruhusiwa kurejea nchini.

Ndugu wa marehemu na waombolezaji wakiwa katika ibada.

Mwanzoni mwa mwaka 2019 hali yake ikabadilika tena, akalazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, ambapo alipatiwa matibabu na baadaye akaruhusiwa na akaendelea na matibabu nyumbani kutokana na afya yake kuimarika.

 

Mwezi Juni hali yake ilibadilika tena na baada ya kufanyiwa vipimo na alibainika kuwa na tatizo la saratani ya tumbo ambapo alitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, mkoani Mwanza, lakini Juni 18, majira ya saa 8:30 usiku, Vaileth aliaga dunia.

Wanakwaya wakiimba nyimbo za maombolezo.

Mwili wa Vaileth utazikwa leo Ijumaa, nyumbani kwao Bupandwamhela katika eneo la makaburi ya familia.

PICHA NA DENIS MTIMA NA IDD MUMBA | GPL

Comments are closed.