The House of Favourite Newspapers

Hofu Vitambulisho vya Taifa Kufutwa

0

Vitambulisho Nida (1)1Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu.

Stori: Mwandishi Wetu, UWAZI

Watanzania bado wapo njia panda kuhusu hatima ya vitambulisho vya taifa, ambapo wengi wanahofia kwamba huenda vikafutwa baada ya hivi karibuni, Rais John Pombe Magufuli kueleza kuwa vitambulisho hivyo havikuwa vimekamilika kutokana na kukosa saini ya mwananchi mhusika.

Vitambulisho Nida (1)-001Mfano wa Kitambulisho cha Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na Uwazi, umebaini kwamba kufuatia kauli hiyo yarais aliyoitoa mbele ya wanasheria katika kilele cha Siku ya Sheria Tanzania, wananchi wengi wameanza kuvipuuza vitambulisho hivyo, wakiitafsiri kauli ya rais kuwa imemaanisha vyote ni feki.

Vitambulisho Nida (3)Mwananchi akijiandikisha

“Sasa kama rais ameshaonesha kwamba kuna kasoro kubwa kwenye vitambulisho kwa kuwa havina saini, unafikiri kuna umuhimu gani wa kuendelea kukaa navyo? Mimi nilishaacha hata kutembea nacho maana naona kinaniongezea tu uzito mfukoni,” Ismail Chuma, mkazi wa Magomeni Mapipa aliliambia gazeti hili.

Vitambulisho Nida (4)Zoezi la uandikishaji

Wananchi wengine waliohojiwa kwa nyakati tofauti, nao walikuwa na hofu kubwa ya uhalali wa vitambulisho hivyo, huku wengine wakienda mbele zaidi na kueleza kwamba haitoshi kuwasimamisha kazi tu watu walioratibu mchakato huo wa upatikanaji wa vitambulisho bali inatakiwa waburuzwe mahakamani.

Vitambulisho Nida (5)Wananchi wakiwa kwenye folleni wakati wa uandikishaji wa kitambulisho cha taifa.

Serikali iliipatia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zaidi ya shilingi bilioni 179.6 kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho hivyo lakini ni walivitengeneza milioni mbili tu mpaka Januari, mwaka huu, hata hivyo vyote havikuwa na saini za wananchi aliyesajiliwa.

Kufuatia ubadhirifu huo na kasi ndogo ya mchakato huo, Rais Magufuli aliingilia kati na kutengua uteuzi wa aliyekuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu (pichani) na kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Mbali na Maimu, Rais Magufuli pia aliwasimamisha kazi maofisa wengine wanne wa Nida akiwemo Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makami, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

Hata hivyo, afisa mmoja wa Nida ambaye hakutaka kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, aliliambia gazeti hili kuwa licha ya kukosa saini kama ilivyoainishwa na rais, vitambulisho hivyo vya taifa vimetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa iitwayo Contactless Smart Card na ndani ya kadi, kuna teknolojia nyingine ya Radio Frequency Induction, inayowezesha kadi kusomwa na mashine maalum kwa kuisogeza tu jirani na mashine hiyo, huku pia ikiwa na taarifa nyingi kwa wakati mmoja kuliko vitambulisho vingine vyovyote nchini.

Malaysia ilikuwa nchi ya kwanza kutumia vitambulisho vya taifa vyenye teknolojia ya kisasa zaidi ambapo vitambulisho hivyo, navyo havina saini kama vilivyo vya Tanzania na badala yake, hutumia alama za vidole (biometric fingerprints).

Leave A Reply