The House of Favourite Newspapers

Homa Ya Matumbo Kwa Watoto, HIVI sasa watu wengi sana, hasa watoto huugua ugonjwa wa matumbo bila kujua kwa nini wanaugua.

DOKTA WA RISASI NA MITANDAO | RISASI| AFYA YA MAMA NA MTOTO

HIVI sasa watu wengi sana, hasa watoto huugua ugonjwa wa matumbo bila kujua kwa nini wanaugua. Ugonjwa wa homa ya matumbo umegawanyika sehemu mbili; vidonda vya ndani ya tumbo (gastric ulcer) au sehemu ya juu ya utumbo mdogo (duodenal ulcer) na husambazwa  na kinyesi cha wanyama kugusana na wanyama wenye maambukizi na kwa binadamu njia kubwa ni kupitia chakula au maji yenye vijidudu vya homa hii ya matumbo ambayo kitaalamu huitwa typhoid.

Wengi wanaougua ni wale ambao hula chakula bila kunawa pia kunywa maziwa ambayo hayajachemshwa, chakula au maziwa yakiwa na vijidudu, basi wote waliokula au kunywa wanapata maradhi haya. Dalili za homa ya matumbo Mgonjwa anaweza akawa anaharisha, kuwa na homa kali na maumivu ya vidonda vya tumboni mara nyingi hukaa katikati, takriban kati ya nusu ya chini na kwenye kitovu na  maumivu ya vidonda vya tumbo mara nyingi hayaishi mara moja pindi yanapoanza.

Dalili nyingine ni kwamba maumivu huongezeka haraka baada ya kula chakula. Mtu anaweza kulalamika kuwa anapata maumivu baada ya chakula. Hii ni kutokana na msisimko wa mnyunyizo wa asidi ambao hububujika kwenye kidonda. Katika vidonda vya duodeni (duodenal ulcer), huchukua takriban

saa mbili hadi tatu ili asidi ifike sehemu ya kidonda. Dalili nyingine ni kusikia kichefuchefu, kichwa kuuma na kutapika. Ugonjwa huu ni hatari sana kwani huweza kushambulia utumbo na kusababisha utoboke na matibabu ya kichelewa huweza kusababisha kifo na asilimia 15 ya wagonjwa wanaougua maradhi haya hupoteza maisha yao.

Dalili zingine ni choo kuwa kigumu kama kinyesi cha mbuzi ,moyo kwenda mbio na kuvimba ini. Pia mgonjwa anaweza asionyeshe dalili zozote lakini akawa na maambukizi na akawa na uwezo wakuambukiza watu wengine. Ugonjwa wa vidonda vya tumbo unaweza kuleta madhara kama vile kuvimba mishipa ya damu, homa ya mapafu na kupata majipu mwilini pia wadudu wa typhoid hushambulia mifupa .

UCHUNGUZI/TIBA

Vipimo vya kugundua wadudu wa typhoid ni kama kuotesha damu na kinyesi pia mkojo unaweza  kuoteshwa ili kugundua aina ya vijidudu. Pia vipimo vya damu kama widal test hutumika na PCR. Matibabu  ni dawa za antibayotiki hutumika kutibu ugonjwa wa typoid ingawa baadhi ya dawa kama  Chlorophenical siku hizi zimeshindwa kutibu kwa sababu ya usugu wa vijidudu.

USHAURI: Ni vema kujikinga na maradhi haya kwa usafi wa chakula na maji tunayokunywa, lazima yachemshwe hata kama ni ya kutoka bombani.

Comments are closed.