The House of Favourite Newspapers

Inawezekana Kuchagua Mtoto wa Kike au wa Kiume

DOKTA WA RISASI NA MITANDAO | RISASI| AFYA YA MAMA NA MTOTO

Watu wengi wamekuwa wakitatizika namna ya kuchagua mtoto wa kike au wa kiume. Habari njema ni kwamba, maendeleo ya sayansi na teknolojia yanazidi kufanya hata yale mambo ambayo awali hayakuwa yakiwezekana, ikiwemo kuchagua jinsia ya mtoto.

Nimeshawahi kueleza kuhusu mada hii lakini kwa sababu ya maombi mengi ya wasomaji, leo nitaifafanua upya. Watu wengi wamekuwa wakishindwa kuelewa jinsi ya kuchagua mtoto wa kiume au wa kike na matokeo yake familia nyingi zimekuwa na uwiano usio sawa kati ya watoto wa kiume na  wa kike. Mara zote inapotokea

mwanamke akawa anajifungua watoto wa kiume tu au watoto wa kike tu, wanaume wengi huanza kulalamika wakiwaona wake au wenzi wao kuwa wana matatizo bila kuelewa kuwa mwanaume ndiye anayesababisha mtoto azaliwe wa kiume au wa kike. Lengo la mada hii ni kutoa utata uliopo katika suala hili kwa kufafanua nini hutokea mpaka mtoto azaliwe wa kiume au wa kike, na pia itakupa mwanga wa jinsi ya kuchagua mtoto umtakaye.

MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANAVYOTOKEA

Wanyama wote, binadamu akiwa mmoja wapo, wana chromosome zinazobeba vizalia (genes) zenye uwezo wa kurithisha tabia na maumbile kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Chembe hizi hupatikana katika muundo wa nyuzinyuzi ndani ya seli za uzazi za mwanaume na mwanamke ( garmetes).  Chromosome hizi zipo za aina mbili tu, X na Y na hizi ndizo zinazosababisha mtoto awe wa kiume au wa kike. Binadamu wa kiume

(Mwanaume) ana jozi ya Chromosome XY wakati mwanamke ana jozi XX.  Wakati wa tendo la ndoa, mwanaume hutoa sperm zenye seli mbili X na Y wakati mwanamke anapokuwa katika siku zake za kuchavusha yai, hutoa yai lenye seli mbili X na X.

Seli moja kutoka kila upande, moja kutoka kwa mwanaume na moja kutoka kwa mwanamke huungana na kufanya jinsia ya mtoto kuwa ya kiume au ya kike. Chromosome moja tu kutoka kwa mwanaume ndiyo inayohitajika kurutubisha yai la mwanamke ili kutengeneza embryo itakayobadilika na kuwa mtoto ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke (Uterus). Itaendelea wiki ijayo.

Save

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.