The House of Favourite Newspapers

Hoteli Jijini Dar es Salaam Yaamriwa Kurejesha Mishahara ya Wafanyakazi

0
Hukumu imetolewa Wafanyakazi walipwe makato ya mishahara yao kutoka mwezi Aprili-Novemba

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Kazi imeiamuru uongozi wa Hotel ya Southern Sun iliyopo jijini Dar es salaam nchini Tanzania kuwalipa wafanyakazi wake 44 asilimia 80 ya mishahara yao ambayo walikatwa wakati wa janga la Uviko-19.

 

Mahakama ilitoa maagizo hayo baada ya kukubali shauri la marekebisho lililowasilishwa na wafanyakazi hao wakiomba kupinga maamuzi yaliyotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambapo uongozi wa hoteli ulishinda.

 

Hakimu Augustine Rwizile alibainisha kuwa makato ya mishahara ya wafanyakazi hao yalianza Aprili hadi Novemba, 2021 ambayo ni jumla ya miezi minane na kwamba wafanyakazi hao walipunguziwa mishahara kwa muda huo bila uhalali.

Hoteli ya Southern Sun

“Wapaswa kulipwa asilimia 80 yao kuanzia Aprili, 2021 hadi Novemba, 2021, maombi haya yana umuhimu maamuzi ya CMA yanafutwa na kuwekwa kando, kwa kuwa hili ni suala la kazi na siamuru gharama yoyote kwa upande wowote”  alisema hakimu.

 

Hakimu Rwizile pia alibainisha kuwa hakuna ubishi kwamba asilimia 80 ya mishahara ya waombaji ilikatwa kwa sababu ya Uviko-19, lakini hakuna ushahidi kwamba kukatwa kwa mishahara hiyo ni maelewano ya pande mbili.

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply