The House of Favourite Newspapers

Htotuba ya Rais Magufuli Akitia Saini Mradi wa Stigler’s Gorge – Video

Rais Dkt.  leo Jumatano, Desemba 12, 2018 ameiaza rasmi safari ya kutimiza ndoto ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kusaini mkataba wa mradi mkubwa wa kufua umeme wa Stiegler’s Gorge.

 

Magufuli na Serikali ya Misri kupitia kwa Kampuni ya Arab Constructors wametia saini mkataba huo ambapo mradi wa Stiegler’s Gorge ndiyo utakuwa mradi mkubwa zaidi kwa Afika Mashariki kwa kuzalisha megawatts 2115 na utagharimu Tsh. Trilioni 6.558.

 

“Mradi wa umeme wa Bonde la mto Rufiji ni wa siku nyingi, ulianza tangu zama za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwenye miaka ya 1970’s, tafiti mbalimbali zilifanywa na upembuzi yakinifu na Nchi ya Norway kuwa mradi huu utatoa megawati 2115 na utazalisha umeme wa kwa zaidi ya miaka 60 ijayo.

 

“Mradi huu utazalishwa kwa gharama nafuu, utakapokamilika utatoa megawati 2115, tunategemea utauuzwa kwa gharama nafuu vilevile, utasaidia kulinda mazingira na kupunguza bei ya umeme. Tutauuza kwa bei ya nchi hivyo bidhaa zetu zitakazozalishwa viwandani tutauza kwa bei ya chini.

 

“Huu ni mradi mkubwa sana utachukua zaidi ya miezi 36 hivyo kabla ya kuaanza utachukua zaidi ya miezi 6 kwa ajili ya kukusanya vifaa kabla ya kuanza. Haiwezekani Viongozi wote wa dini waliokuja hapa kushuhudia halafu Mradi ushindwe kukamilika na isitoshe wanaoutekeleza wenyewe ni kule ambako Yesu alikimbilia,” amesema Magufuli.

Comments are closed.