Hukumu ya Malinzi Yakwama, Hakimu Ahamishwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kusoma hukumu ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu kwa sababu hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, Maila Kasonde amehamishwa kikazi hivyo hukumu hiyo bado haijakamilika.

 

Kesi hiyo imeahirishwa leo Alhamisi, Novemba 7, 2019 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kevin Mhina hadi Novemba 21, mwaka huu kwa ajili ya kusomewa hukumu.

 

Malinzi pamoja na wenzake wanakabiliwa na mashitaka mbalimbali ikiwemo kughushi na kutakatisha fedha kwa nyakati tofauti.

 

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na aliyekuwa katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania, Celestine Mwesigwa, Karani Frola Rauya pamoja na Mhasibu Nsiande Mwanga.

 
Toa comment