The House of Favourite Newspapers

Huyu Kanoute ni Mtu Babake

0

KWA mara ya kwanza msimu huu, Simba wamewaonyesha mashabiki wao kuwa wanauwezo wa hali ya juu uwanjani.

 

Simba walikuwa kwenye maandalizi ya msimu nchini Morocco na baadaye wakaenda Karatu Arusha na hawakuwahi kuonekana mbele ya mashabiki, bali jana ndiyo ilikuwa siku ya kwanza wakati wakicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki kwenye Tamasha la Simba Day, dhidi ya TP Mazembe.

 

Wakati Simba wanatangaza kuwa watacheza na TP mashabiki baadhi yao walipata hofu kutokana na kiwango cha Wacongo hao ambao wamewahi kuchukua Klabu Bingwa Afrika mara tatu, lakini wengine wakasema ndiyo kipimo chao sahihi na kweli jana Simba waliupiga mwingi dhidi ya TP Mazembe na kumaliza mechi hiyo kwa Simba kulala kwa bao 1-0.

 

Matokeo hayakuwa ishu sana, bali kiwango ambacho kilionyesha na Simba ambayo kwa mara ya kwanza walicheza kwenye Dimba la Taifa wakiwa mbele ya mashabiki 60,000 na zaidi, bila Clatous Chama na Luis Jose Misquoinne ambao wamewauza.

 

Hata hivyo, kiwango waliichoonyesha, Saidio Kanoute, Kibu Denis,Peter Banda na Pape Sakho kilitosha kwa mashabiki wao kuamini kuwa hakuna tena pengo la wawili hao.

 

Simba ambao walianza na kikosi chao cha zamani isipokuwa wachezaji wawili tu, Kanoute na Denis walicheza kipindi cha kwanza kwa umakini mkubwa, huku Kanoute akitakata kwenye eneo la kiungo mshambuliaji, ambapo aligusa mpira mara 16 na aliupoteza mara moja tu.

 

Kiungo huyo mwenye umbo dogo, alionyesha umahiri mkubwa wa kupita katikati ya mabeki na kuwasumbua sana viungo wa Mazembe ambao wana uzoefu wa kucheza michezo ya kimataifa.

 

Mbali na mipira aliyogusa, pia alifanikiwa kuchezewa madhambi mara mbili kwenye mchezo huo ambapo alitoka dakika za mwisho sana na kumpisha Jonas Mkude lakini akionyesha atakuwa msaada mkubwa kwa Simba.

 

Mbali na huyo kiwango kingine bora kilionyesha na Denis ambaye amesajiliwa kutokea Mbeya City, ambapo alionekana kuwasumbua sana mabeki wa Mazembe kutokana na kucheza kwa kutumia nguvu sana lakini pia alionyesha kiwango cha juu cha kupiga mashuti.

 

Banda na Sakho ambao waliingia mwishoni walionyesha ubora wa juu lakini kilichowagharimu ni muda mchache waliotumia uwanjani.

 

Hata hivyo, kiwango cha mechi kwa timu zote kilikuwa cha kimataifa ambapo timu zote zilifanikiwa kuonyesha ubora wa juu sana na sasa kinachosubiriwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga wikiendi ijayo.

NA ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Leave A Reply