The House of Favourite Newspapers

Huyu Naye..! Fuata Maelekezo – 13

0

ILIPOISHIA GAZETI LA RISASI JUMAMOSI:

“Wewe nani?” aliuliza kwa ukali mama Rehema…
“Mimi Jamila mama.”
“Jamila gani na wa wapi?”
Nilishangaa sana kuulizwa hivyo…
“Mimi Jamila mfanyakazi wako wa ndani mama, nilikuaga nakwenda saluni kutengeneza nywele.”
SASA TAMBAA NAYO MWENYEWE…

“Mh! Mbona sikukumbuki…Jamila…Jamila…Jamila! Ulikuwa unaishi humu kwangu?” eti mama Rehema aliniuliza swali hilo…
“Mama mimi Jamila hunijui wakati nimetoka jioni hii hapo nyumbani kwako kwenda saluni, ni haki kweli kuniuliza hivi?”  nilisema kwa sauti ya juu kidogo na iliyoashiria hasira fulani hivi…
Nilibaini kwamba, mama Rehema alitaka kwa makusudi kuniweka nje kwenye kibaridi lakini si kweli kwamba alikuwa hanijui au hanikumbuki!
Mara,  baba alitokea…
“Nimesema mimi sikukumbuki na wala sijawahi kuwa na mfanyakazi anaitwa Jamila hapa nyumbani kwangu. Labda umepotea njia, jiangalie sawasawa.”
Baba alisikia kila kitu alichokisema mke wake, lakini akauliza…
“Vipi wewe mbona upo nje?”
Kabla sijamjibu, mama Rehema akafungua geti haraka sana…
“Nimekusikia ukisema huna mfanyakazi anaitwa Jamila humu ndani?” baba Rehema alimuuliza mama Rehema…
“Huyu binti ameanza kufanya umalaya wake hapahapa nyumbani kwangu, namshangaa sana. Ameondoka hapa saa ngapi sijui ile, nadhani mchana, saa hizi ndiyo anarudi,” eti mama Rehema alinisemelea kwa mume wake…
“Sasa wewe umejuaje alikwenda kufanya umalaya?” baba Rehema aliuliza, mimi nikadakia…
“Eti…”
“Baba Rehema tangu saa sita mchana!”
“Mimi nilipokuja ilikuwa saa sita mchana, si nilikuja saa tisa sijui, nikaondoka na kumwacha.”
Mama Rehema uso ulimshuka, lakini akakomaa na mimi…
“Hata kama aliondoka saa kumi na moja ndiyo arudi muda huu?”
“Kwani aliaga anakwenda wapi?” baba Rehema yeye alikuwa mtu wa mashuti tu, maana si tulikuwa wote bhana! Hapo sasa tulishafika sebuleni…


Alisema anakwenda saluni eti.”
Baba Rehema aliachana na mimi na mkewe akaenda chumbani, alipotoka tayari alikuwa ndani ya vazi la bukta mtumbo wazi!
“Chakula,” alisema kwa sauti baba Rehema huku akikaa kwenye kochi sebuleni…
“Chakula bado, si huyu Jamila aliondoka,” mama alijitetea kwa kuondoka kwangu…
“Hayo ni maneno gani mama Rehema? Jamila kuondoka ndiyo hapa nyumbani hatuli, ni sahihi kweli? Kwa hiyo mimi mke wangu ni Jamila sasa, niambie nijue moja,” alifoka baba, mama Jamila akawa kimya…
“Jamila,” baba Rehema aliniita…
“Abee…”
“Nipikie chakula nile mama.”
“Sawa baba.”
Tuliitana kwa heshima, lakini nyuma yake tulikuwa na mambo yetu wenyewe…
“Acha nitapika mwenyewe,” mama Rehema aliniambia kwa sauti ya chini baada ya kunifuata jikoni…
“Jamila,” baba Rehema aliniita tena akiwa sebuleni mimi jikoni…

“Abee baba.”
Ile naanza kwenda tu, mama Rehema akanishika gauni…
“Marufuku kuitika baba, kwa nini usiseme baba Rehema?”
“Mama! Yaani nimwitikie abee baba Rehema?”
“Ndiyo.”
“Mh!”
“We Rehema…”
“Abee baba Rehema,” niliitika nikiwa nimeshatoka jikoni…
“Kuitika gani huko? Kwani mpaka useme baba Rehema? Kwa asiyejua kuwa mimi ni baba Rehema nani?” baba Rehema alinifokea…
“Mama ameniambia niwe naitika hivyo.”
“Amekwambia saa ngapi?”
“Sasa hivi ulivyoniita kwa mara ywa kwanza nikasema abee baba.”
“Kaa hapa,” aliniambia baba Rehema huku akishika sehemu ya kochi ambapo ni karibu sana na yeye…
“Mama atatukuta bwana,” nilimwambia baba Rehema kwa sauti ya chini sana…
“Nimesema kaa,” na yeye aliniambia kwa sauti ya chini, nikakaa…
“Unanipikia nini?” aliniuliza.
“Mayai, pia kuna samaki nitampasha moto nitaleta na mkate, lakini mama kaniambia atapika yeye.”
“Mama Rehema,” baba Rehema alimuita…
“Abee baba.”
Nilitaka kusimama, lakini baba Rehema akanizuia kwamba nikae tu.
Mama Rehema alipotokea, kwanza alisimama ghafla na kujishika kinywa kwa mshangao. Hajawahi kuniona nimekaa na mume wake hata siku moja…
“Baba Rehema ndiyo nini?” alimuuliza…
“Namuuliza ananipikia nini?”
“Ndiyo akae jirani na wewe kiasi hicho?”
“Umemhalalisha wewe mwenyewe. Nimeuliza chakula, ukasema hakijapikwa kwa sababu Jamila alikuwa hayupo! Sasa mimi nimchukulie Jamila kama nani? Si kama mke wangu!”
Mama Rehema alikuja mbio, akanishika mkono na kunivuta…
“Nije nikuone siku nyingine,” alisema…

“Umuone kwani hapa amekaa yeye au mimi ndiyo nimetaka akae,” alisema baba Rehema kwa sauti ya upole.
Mama Rehema alirejea jikoni huku akiniacha mimi sebuleni, nimekaa kwenye kochi lingine.
Tulikutana macho na baba Rehema, akaachia tabasamu na mimi nikaachia la kwangu, tukakaziana macho, nikayaona ya kwake yanaanza kulegea na mimi nikayalegeza ya kwangu, nikamwona anasimama, ananifuata nilipokaa, akakaa pembeni yangu, akanikumbatia kweupee kabisa aka…

Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi ijayo.

Leave A Reply