The House of Favourite Newspapers

Huyu Naye..! Fuata Maelekezo-11

0

ILIPOISHIA GAZETI LA RISASI JUMAMOSI:
“Sawa baby wangu, nakupenda sana,” nilisema nikamwongezea na zaidi kisha nikasimama na kwenda kumpa denda, akalikubali, tukajikuta tukiganda humo kwa muda.
Tuliganda tukashtuka baadaye, baba Rehema akasema…
“Umenikumbusha mbali, sasa unaweza kutoka humu ndani ukasingizia unakwenda saluni kuseti nywele?”
SHUKA NAYO…

“Naweza, nitamwambia mama.”
“Umwambie, halafu ukishatoka unipigie simu haraka sana,” alisema baba Rehema akiondoka na kufunga mlango mkubwa.
Nilikwenda kuoga, nilipotoka, kwenda chumbani kwangu nikakutana na mama akitoka huku akionekana kuwa na uso wa aibu, sikujua alifuata nini.
Lakini nilipoingia chumbani na kukuta mazingira yakiwa vululuvululu ndiyo nikajua alikuwa akichangua vitu…
“Sasa hapa mama Rehema alikuwa akitafuta nini jamani?” nilijiuliza mwenyewe…
“Ahaa! Huyu alikuwa akitafuta simu yangu,” nilibaini mwenyewe moyoni. Kumbe mwenzake nilikwenda na simu bafuni kuoga kwani najua lazima mama atakuwa anaisaka ili aone nawasiliana na nani!
Nikacheka kicheko cha kejeli tena kwa nguvu, huenda alinisikia kule alipo.
Nilivaa, nikatoka, nikamkuta sebuleni lakini aliponiona aliangalia pembeni na hakuwa mkali kama ilivyo kawaida yake. Alijua nimebaini alichokifanya chumbani kwangu…
“Mama samahani, naomba uniruhusu niende saluni.”
“Wapi?” aliniuliza kwa mkato akiwa haniangalii…
“Popote pale.”
“Baba Rehema kaondoka?”
“Ndiyo.”
“Kasema anakwenda wapi?”
“Kazini.”
“Nenda uwahi kurudi,” aliniambia.
Niliondoka nikiwa na amani, maana sikukutana na ukuta wakati wa kuomba ruhusa hiyo.
Nilipotoka getini tu, nikaanza kutembea kuelekea barabarani huku simu ikiwa sikioni…
“Haloo…nimeshatoka,” nilimwambia baba Rehema kwa njia ya simu.
“Oke…oke sasa sikia, tembea hadi kituoni, panda daladala uje kushuka kwenye kituo kinachofuata, kuna kibanda cha kuuza juisi hapo kituoni,” alinielekeza.
“Sawa.”
Nilipanda daladala, nikaenda kushuka kituo alichoniambia baba Rehema, kwa pembeni nikamwona amekaa kwenye baa nikamfuata hapohapo…
“Karibu sweet,” alinikaribisha baba Rehema.
Baada ya kukaa, nikachezesha macho kuwaangalia wateja wengine pale baa, karibu wote walikuwa wakiniangalia mimi, sikujua kwa nini, maana si kwamba nilikuwa mdogo sana, halafu mimi nina umbo la kimamamama.
Ukimwangalia baba Rehema na mimi huwezi kusema ni mtu na mtoto wake wa kumzaa…
“Mbona watu wananiangalia sana?” nilimuuliza baba Rehema nikijifuta jasho kwa kitambaa…
“We uko poa Jamila, unadhani ndani ya baa hii kuna mwanamke anakufikia kwa uzuri…. hakuna mi nakwambia,” baba Rehema aliniambia, nikacheka kwa mbali sana…

Nikuhudumie nini?” mdada mmoja, alisimama pembeni yangu akiwa ameshika sinia na opena, nikajua baamedi.
“Soda…”
“Soda gani?”
“Kwani kuna soda gani?” nilimuuliza.
Kabla hajajibu, baba Rehema ambaye alikuwa akituangalia, akadakia…
“Mpe bia huyu…”
“Aaah! Baba Rehema, bia tena?!”
“Moja tu tosha.”
Nilimwangalia baamedi kwa macho ya kumwambia sawa lete bia…
“Bia gani?” akaniuliza baamedi…
“Yoyote…”
“He! Yoyote?” baamedi alishangaa, hata mimi nilishangaa…
“Ndiyo, yoyote!” baba Rehema alirudia…
“Haya, ya moto ya baridi?” baamedi aliuliza tena akitaka kuondoka.
“Yoyote!” baba Rehema alisema tena, baamedi akacheka huku akiondoka…
“Siwezi kulewa?” nilimuuliza baba Rehema nikiwa nakaa vizuri…
“Huwezi, kwani hujawahi kunywa?”
“Hata siku moja.”
“Kweli?”
“Kabisa…sijawahi kunywa. Lakini sidhani kama naweza kulewa. Kwani kawaida mtu analewa bia ngapi?”
“Wanasemaga saba, nane,” baba Rehema aliniambia, nikashangaa kwani yeye mwenyewe nilimkuta anakunywa bia, ina maana hajui analewaga ngapi?!
“Bia ilikuja, nikaifuta, nikaletewa nyingine, nikaifuta, nikaona silewi, nikaletewa nyingine, nikaifuta.
Sasa kwenye kusimama kwenda chooni ndiyo nikajua ujinga wangu, nikayumba na kupiga mwereka puu! Baba Rehema akaniwahi…
“He! Jamila vipi tena?”
Kumjibu nilishindwa kwani kila nilipotaka kuinua midomo, iligoma. Nilipofumbua macho nikahisi watu wote ninaowaona, waliokaa, walikuwa miguu juu kichwa chini na waliosimama pia hivyohivyo.
Nilipoangalia mbele kwenye viti nikaona vinakuja kuniangukia kichwani, nikalala ili kukwepa visinifikie. Nilimsikia mtu mmoja akiuliza…
“Au amekunywa bia zenye sumu?”
“Hamna, huyu alisimama kunywa bia leo ndiyo ameanza tena,” alijibu baba Rehema, nikataka kusema muongo huyo, leo ndiyo mara ya kwanza, nikashindwa.
Wengine walitoa ushauri nirudishwe nyumbani, hapo ndipo nilipokumbuka nitakachokwenda kutendewa na mama Rehema kwa kugeuza saluni kuwa baa…
“Jamila, tuondoke tafadhali,” alisema baba Rehema. Nikatingisha kichwa kukubaliana naye kisha akasema tena…

Lakini wewe siwezi kukupeleka nyumbani moja kwa moja, lazima ukapumzike kwanza mahali, sawa?” pia nikamkubalia kwa kutingisha kichwa.
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi ijayo.

Leave A Reply