The House of Favourite Newspapers

Huyu Naye..! Fuata Maelekezo-14

0

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
Nilipotoka chooni, niliamini mama Jamila hayupo kwani ukimya ulikuwa mkubwa, nikasema moyoni huu ndiyo wakati wangu mimi na baba Rehema. Nikarudi chumbani, nikafunga mlango maana baba Rehema alishatangulia kitandani…
“We Jamila.”
TAMBAA NAYO MWENYEWE…

Sauti hiyo ilikuwa ya mama, nilishtuka sana. Nikahisi kupepesuka…
“Abee mama.”
“Baba Rehema amekuaga?”
“Hapana mama,” nilijibu huku nikimwangalia baba Rehema pale kitandani…
“Sasa atakuwa amekwenda wapi?”
“Ndani hayupo?” nilimuuliza kinafiki mama Rehema.
“Hayupo, sijui atakuwa amekwenda wapi?”
Nilianza kuhisi kwamba, mama Rehema alijua mume wake yuko chumbani kwangu ila alishindwa namna ya kuniingia ili kujionea mwenyewe…
“Au amekwenda kunywa bia zake pale baa?” eti mama Rehema ambaye ndiye mwenye mke, aliniuliza mimi badala ya mimi nimuulize yeye…
“Labda.”
Mazungumzo yake hayo aliyatoa akiwa amesimama nje ya mlango wangu. Ina maana alikuwa hataki kutoka ndiyo maana nikasema alikuwa na wasiwasi…
“Haya usiku mwema mama,” niliamua kumuaga huku nikitega masikio kumsikia atasema nini.
“Unalala?” aliniuliza.

“Ndiyo mama.”
“Mh! haya,” aliguna na kumalizia maneno hayo.
Nilikuwa na wasiwasi sana, jasho jembamba lilinitoka huku nikijua kwamba tumebambwa tayari na hilo halina ubishi.
Sikumsikia mama Rehema akitembea kuondoka nje ya mlango wangu. Kwa maana hiyo, alikuwa bado amesimama akinisikilizia.
Nilipanda kitandani nikitetemeka sana, nikamwambia baba Rehema kwa sauti ya chini sana…
“Amejua we upo ndani!”
“Achana naye,” alisema baba Rehema akijifanya hajali wala haogopi. Mwenzenu yule baba sijui alikuwa anajiamini nini.
Ghafla  mama Rehema akagonga mlango…
“Ngo ngo ngoo.”
“Nani?” niliuliza nikijua ni yeye. Ilibidi niulize ili kumpoteza maboya ajue sikuwa na wazo na yeye tena…
“Mama Rehema naongea…Jamila,” aliita.
“Abee mama.”
“Hebu fungua mlango nikwambie kitu.”
Baba Rehema alinishika, akanivutia kwake. Nikajua anataka kuniambia kitu, nikamwinamia mpaka sikioni…
“Usifungue mlango,” baba Rehema aliniambia hivyo. Lakini mimi niliona ugumu, nikisema nisifungue ina maana atakuwa na uhakika yeye yumo ndani na anaweza kukesha nje ya mlango, nikamwambia…
“Mimi nafungua, wewe ingia chini ya kitanda haraka,” wakati nasema hivyo tayari nilikuwa natoka kitandani.
Baba Rehema alipoona msimamo wangu, mwenyewe alitoka kitandani na kuzama mvunguni. Mimi nikafungua mlango…
“Naweza kuingia ndani?” mama Rehema aliniuliza huku akinikazia macho maana nilipofungua mlango, nilisimama katikati…
“Sawa,” nilisema nikimpisha.
Alipita, akaenda kukaa kitandani huku akizungusha macho yake kila kona ya chumba…
“Unajua Jamila mimi siku hizi simuelewi baba Rehema. Amekuwa na tabia tofauti sana. Akipanda kitandani muda mwingine yeye anachati na simu tu mpaka nataka kulia.
“Naamini hizi salama zangu utampa ili ajue kuwa, hanitandei haki,” alisema mama Rehema akasimama kuondoka…
“Sasa mama mimi nitampa salamu baba Rehema kama nani yangu kwa mfano?”

“Utajua mwenyewe na huo mfano wako,” alinijibu akifunga mlango kwa nguvu ukajibamiza paa!
Sasa ndiyo nikamsikia akitembea kuelekea kwake. Sikujua kama alisema vile baada ya kubaini mumewe hayumo ndani kwangu au alijua yumo lakini alijificha mvunguni.
Nilisonya, nikasimama na kufunga mlango huku baba Rehema atoka kule chini…
“Nilitaka nitoke, ana bahati sana. Hawezi kuja kueleza mambo yangu kwako. Kwa nini aliamua kusema vile?”
“Mimi sijui, mnajuana wenyewe wewe na mke wako. Labda amejua umejificha chini ya kitanda change.”
Licha ya dalili zile lakini cha ajabu, baba Rehema hakutaka kuondoka kurudi kwa mke wake, akasema ni lazima tulicheze gemu kwanza ndipo aondoke akiwa na amani…

“Sasa baba Rehema, je mkeo akirudi?”
“We mlango umefunga au uko wazi?”
“Nimefunga.”
“Sasa wasiwasi wako uko wapi?” alisema baba Rehema akiwa ananiandaa tayari kwa kuingia uwanjani.
Kipyenga kilipulizwa, mchezo ukaanza lakini ukimya ulitawala zaidi na vitendo ndiyo vilichukua nafasi kwani muda mwingi tulikuwa tukimsikilizia mama Rehema kama atakuja.
Kuna wakati si nikawa najisahu bwana, nikawa napayuka lakini nikajizuia kwa nguvu zangu zote japokuwa hali hiyo nayo ilikuwa inanikata stimu ya mchezo wenyewe maana hitimisho la mchezo ni mashabiki kushangilia.
Mimi sijui nini kilitokea mwenzenu, lakini nilijikuta nikipayuka bila kujali kama nitasikika au la huko nje lakini huku mlango wa chumbani kwangu nao ukigongwa kwa nguvu…
“Ngo ngo ngoooo!”
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi ijayo.

Leave A Reply