The House of Favourite Newspapers

Huyu naye…fuata maelekezo-3

0

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
“Kwani we mama Rehema hujajua kuwa, wengi katika kusalimia wale wenye umuhimu mkubwa ndiyo wanakuwa wa mwisho? Kwa sababu najua lazima utaniuliza za kazi, utanipa pole, utanipongeza kwa kazi nzuri na utaniambia lolote la hapa nyumbani…”
“Lolote la hapa nyumbani ni huyu Jamila, ananitafuta sana. Hajui kama mimi ni bosi wake…mimi nahisi amechoka sasa, anataka kuacha kazi arudi kwao,” alinisema mama Rehema mpaka nikaanza kutetemeka.SHUKA NAYO SASA…

Nilijiuliza kosa langu kwa mama ni lipi hasa?! Maana kila nilipojaribu kukumbuka wapi nilimtendea mabaya sikupata jibu!
***
Wiki mbili zilikatika, siku hiyo nakumbuka ilikuwa asubuhi ya Jumapili, hakuna aliyekuwa anatoka nyumbani. Si baba Rehema wala mkewe mama Rehema na Rehema mwenyewe ndani.

Niliwaandalia chai na magimbi, mama Rehema akaniambia niweke na mchuzi wa nyama na vipande vyake vya jana, nikaenda kuvichemsha, nikavitenga mezani…
“Jamila,” aliniita mama wakati wameanza kunywa…
“Abee mama…”

“Hakuna juisi ya ukwaju?”
“Ipo mama…”
“Lete… Halafu jana pia si dagaa walibaki?”
“Ndiyo mama.”


Walete, pasha moto walete…vipi ulimaliza zile firigisi?”
“Zipo mama…”
“Lete pia…”
“Hivi we mama Rehema vyakula vyote hivyo unavyokula huoni unavyonenepeana?” baba Rehema alimuuliza mke wake…

“Kwa hiyo unataka niwe mwembamba kama Jamila siyo? Yaani wewe unapenda mwanamke mwenye umbo kama Jamila msichana wako wa kazi…hausigeli?” mama Rehema alianza kuwaka ile mbaya huku akimkazia macho mume wake…

“Hayo ya Jamila yamekujaje sasa? Mimi nimemzungumzia Jamila na mwili wake au wewe na kulakula kwako? Halafu we mama Rehema jaribu kuwa na heshima hata ndogo kama mbegu ya mchicha….ukiendelea na tabia yako hiyo nitakuja kufanya maamuzi magumu sana.”
“Wewe ndiyo sababu…utaniambiaje mimi kwamba nanenepeana kwa sababu ya kulakula..?”
“Kwani uongo?” aliuliza baba Rehema huku akisimama, akaenda uelekeo wa chooni. Nadhani akaenda chooni kabisa.

Kuna wakati nikaenda kumwaga maji machafu nje uani, nikakutana naye wakati narudi sasa…
“Jamila,” baba Rehema aliniita kwa sauti ya chini akiwa amesimama mbele yangu kiasi kwamba mimi nisingeweza kupita kutokana na upenyo kuwa mdogo…
“Bee…”

“Hivi mama Rehema mzima kweli?”
“Mh! Baba we acha tu…mimi mwenyewe namshangaa sana kwa kweli…”
“Da! Yaani siku hizi amebadilika sana,” alisema baba Rehema…
“Baba siajabu hajabadilika…”

“Bali..?”
“Bali amerudia tabia yake ya asili.”
Nilimwona baba Rehema akitingisha kichwa kama aliyekuwa akisema…
“Ni kweli kabisa.”

Akapinda kidogo ili nipite, wakati napita, tukawa sambamba, akanishika mkono…
“Vipi tena baba?” nilimuuliza huku nikimwangalia kwa macho laini…
“Hivi una miaka mingapi vile?” aliniuliza baba…
“Ishirini na nne.”

Niliamua kudanganya maana ukweli ni kwamba nilikuwa na miaka ishirini na moja lakini nikajizeesha kwa makusudi ili nimsikie anataka nini..!

Sawa. Umewahi kuwa na mwanaume?” aliniuliza lakini kabla sijamjibu, mama akaniita…
“Abee…”
“Lete kile kipande cha fenesi.”

“Duu!” nilijikuta nikiguna kwa sauti ya chini sana ili asisikie ikawa kiama changu mie…
Nilichukua kipande cha fenesi nikampelekea…
“Lete na kile kipande cha samaki nilichosema uniwekee kwenye oveni.”
“Sawa mama.”

Nilimchukulia kipande cha samaki nikampelekea huku moyoni nikimcheka sana. Huyu mama Rehema alikuwa kiboko sana kwa msosi.
Baada ya kumpa samaki niliamua kutoka nje ili kuangalia kama naweza kukutana na baba Rehema tumalizie mazungumzo. Nadhani na yeye alikuwa akinisubiri kwani alikuwa kwenye mlango wa uani…

Baba sijawahi kuwa na mwanaume. Kwani umesikia nini baba? Mimi hata nikienda gengeni wakinitongoza huwa nawakataa, nawaambia sitaki…”
“Oke…oke…nitakwambia kitu kama tukibaki wawili tu,” baba Rehema aliniambia, nikakubali na kuendelea na kazi zangu.

Kesho yake ilikuwa Jumatatu, lakini jioni ya kama saa kumi na mbili. Baba Rehema alirudi na kukuta mkewe amekwenda saluni, Rehema alikuwa amelala chumbani kwake…
“Shikamoo baba,” nilimwamkia kwa bashasha kwani nilijua nipo huru…
“Njoo uniamkie karibu hapa,” alisema akininyooshea mkono wa kuniita. Nikaenda…
“Shikamoo baba…”

“Marhaba za hapa?”
“Nzuri…”

“Njoo ukae hapa kidogo basi Jamila jamani,” alisema baba Rehema huku akinishika mkono na kunikalisha kwenye mapaja yake. Nilijisikia aibu sana yaani mtu mzima kama mimi kukalishwa kwenye mapaja kama mtoto…! Aaaa! Haiji! Lakini nilikaa…
“Umekula?”
“Ndiyo…”
“Oke…sasa nikwambie kile kitu nilichosema jana nitakwambia?”

Je, nini kitaendelea? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi.

Leave A Reply